Hirizi yaleta bifu kati ya Chege na Mtangazaji Maimartha wa Jesse

Picha ya Chege na Temba iliyozagaa mtandaoni yaleta chuki kati ya Chege na Miamartha, baada ya mtangazaji huyo kuweka Instagram picha hiyo iliyozungushiwa alama nyekundu kwenye mkono wa Chege ikionyesha kitambaa cheusi alichokuwa kajifunga na kuuliza kama ni Hirizi. 
Kwa mujibu wa Chege, Picha hiyo ilipigwa alipokuwa akifanya show wiki iliyopita mjini Dodoma, na kitambaa hicho si hirizi, bali ni kitambaa cheusi alichofunga kuashiria kuguswa namsiba wa Mez B, kwani amefariki asubuhi wakati wao walikuwa na show mchanawa saa tisa.


"Ukitaka kujua ile picha ipoje  inabidi usome tshirts za Chege na Temba zimeandikwa nini, yah, zimechorwa chorwa kwa maker pen zimeandikwa RIP Mez B. Kitu tulichokifanya pale nikama tulichokifanya Musoma, baada ya lile basi lililouwa watu kibao.kitu ambacho kilichotokea Dodoma, tulikuwa na tamasha saa tisa mchana, sisi tumefika dodoma siku moja kabla ya tamasha, kwahiyo siku ya tamasha ambalo lilikuwa linafanyika saa tisa mchana lakini asubuhi tumeletewa taarifa saa tano asubuhi kuwa Mez B amefariki tukiwa pale pale dodoma........" amesema Chege

sisi tumeenda kwenye tamasha tukaona nini tunafanya leo, kuna msiba, Mez B kwao dodoma, inabidi tuvae tshirt, vitambaa vyeusi kuashiria kuna msiba, kina Byser walivaa tshirt nyeusi, raba nyeusi kuashiria kama kuna msiba, watu wanatumia tu mitandao vibaya, Instagram inatumika vibaya, instagram imekuw kama bbm imekuwa kama Facebook.wanautumia mtandao vibaya, wanaandika vitu ambavyo hawajui kwanini vinafanyika. Mimi ni akili,  nina busara, nina upeo, nina experience kubwa kwenye game, ningekuwa nafanya vitu ambavyo wanandika nisingevifanya hadharani. Mimi naamini watu wamenikose.....haijaniathiri kwasababu najua hakuna ukweli wowote....."aliendelea Chege



Mtangazaji wa kitambo, maimartha Jesse aliitupia picha hiyo kwenye acc yake ya IG na kuandika, 

"Angalia mkono Wa kushoto Wa chegge @chegechigunda hiiii ni hirizi ? any way isiwe kesi jiachie chege ila mziki mziki wako naupenda hata ukiniroga sawa Tu...japo cna imani hiyoo ."

Chege ameongea na Clouds Fm juu ya caption hiyo

"...Maimartha wa Jesse mi sio mtu wa kuvaa hirizi, mimi nimevaa kwasababu  ya msiba wa msanii mwenzangu men, mvaa hirizi anavaa hirizi mchana??... halafu chuki unajua haijengi, chuki inamfanya mtu anazidi kufanikiwa, chuki ambayo haina msingi....... namshangaa mtu kama maimartha ananiandikia ushamba Maimartha?? mi namuheshimu miaka yote lakini sasa naona kama anataka nimuoneshe na mimi ni mtoto wa kihuni vile vile. Maimartha na mimi wapi na wapi rafiki yangu, Maimartha unaandika kwenye ma Instagram?? unajua ushamba sio kuzaliwa kijijini? ushamba ni kutokujijua kama unachemsha... Mitandao tumia upate hela, tumia mitandao kwa biashara zako. unatumia mitandao kutangaza dawa za kuongeza matako, unatumia mitandao kuongeza dawa za kujichubua ngozi inabadilika inakuwa ya blue kila siku." amesema Chege



Naye Maimartha Jesse akizungumzia suala hilo alisema kuwa hakuwa na nia mbaya ndiyo maana aliuliza ili watu wamwambie ni kitu gani amevaa Chege na mwisho alimuomba msamaha Chege baada ya kumkwaza kwa tukio hilo.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment