Test Feature Post 1

Ea eam labores imperdiet, apeirian democritum ei nam, doming neglegentur ad vis. Ne malorum ceteros feugait quo, ius ea liber offendit placerat, est habemus aliquyam legendos id. Eam no corpora maluisset definitiones, eam mucius malorum id. Quo ea idque commodo utroque, per ex eros etiam accumsan.
Read more

Test Feature Post 3.

Ea eam labores imperdiet, apeirian democritum ei nam, doming neglegentur ad vis. Ne malorum ceteros feugait quo, ius ea liber offendit placerat, est habemus aliquyam legendos id. Eam no corpora maluisset definitiones, eam mucius malorum id. Quo ea idque commodo utroque, per ex eros etiam accumsan.
Read more

Test Feature Post 4.

Ea eam labores imperdiet, apeirian democritum ei nam, doming neglegentur ad vis. Ne malorum ceteros feugait quo, ius ea liber offendit placerat, est habemus aliquyam legendos id. Eam no corpora maluisset definitiones, eam mucius malorum id. Quo ea idque commodo utroque, per ex eros etiam accumsan.
Read more

Welcome To iProperty Themes !

Sunday, January 4, 2015

Wednesday, December 17, 2014

BALOZI KAMALA AKARIBISHWA JIJINI WETTEREN UBELIGIJI

Posted 2:17 PM | Posted by sunday succi


Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akilisikiliza maelezo kuhusu zawadi aliyokabidhiwa kama ishara ya kumkaribisha jijini Wetteren Ubeligiji. Anayetoa maelezo ni Mhe. Live De Gelder Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii jijini Wetteren. Balozi Kamala leo atatembelea viwanda mbalimbali jijini Wetteren na atakutana na Wafanyabiashara kuel

TALIBAN WAUA WATU 126 WAKIWEMO WANAFUNZI ZAIDI YA 100 NCHINI PAKISTANI

Posted 2:13 PM | Posted by sunday succi


Majeruhi katika shambulio hilo wakipatiwa huduma za kitabibu.

ZOEZI LA UANDIKISHA WAPIGA KURA KIELEKTRONIKI (BVR), KWA MAJARIBIO LAANZA DAR

Posted 2:11 PM | Posted by sunday succiZoezi la kuandikisha upya wapiga kura wenye sifa, kwa kutumia mfumo mpya wa kidigitali au kielektroniki, yaani Biometric Voters Registre, (BVR), limeanza jijini Dar es Salaam kwa majaribio, na hakika hakuna longolongo wala kupoteza muda, Mimi nimeshuhudia mtu mmoja humchukua takrivan dakika 10 tu kupatiwa kitambulisho au kadi ya kisasa ya kupigia kura. Hatua hizo ni kama zifuatazo, mosi, mtu anayeomba kuandikishwa ataonyesha kitambulisho na kujaza fomu ya Tume ya Uchaguzi ya kuomba kuaandikishwa, baada ya kujaza fomu hiyo hatua ya pili ni kuipeleka kwa muandikishaji msaidizi namba 2 ambaye ataingiza kumbukumbu hizo zilizomokatika fomu kwenye computer, hatua itakayofuata ambayo ni ya tatu, mtu huyo atatakiwa kuweka dole gumba na vidole vyake vitano ili viweze kuchukuliwa alama zake yaani scanned, baada ya hapo hatua inayofuata ni muombaji kupigwa picha na mwisho kabisa ni kupatiwa kikadi yaani kadi ya kupigia kura, kwa hakika inafanana sana na kitambulisho cha taifa, kama umekwishakipata. Zoezi hilo kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC, litaanza rasmi nchi nzima kuanzia Februari mwaka 2015 ambao ndio mwaka wa uchaguzi mkuu
Mwandishi msaidizi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa, (NEC), ambaye kwa sasa watajulikana kama BVR Operators, akijaza fomu ya mtu anayeomba kuandikiswa kupiga kura leo Jumanne Desemba 16, 2014, plae Bunju A, wilaya ya Kinondoni jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam
Muombaji (Kulia), akijaziwa fomu kabla ya kuendelea na hatua zingine
Muombaji (Kulia), akikabidhi fomu aliyojaziwa katika hatua ya kwanza ya kuomba kuandikiswa

DIAMOND NA KUNDI LAKE WALA CHAKULA NA WATOTO YATIMA MOMBASA NCHINI KENYA

Posted 2:10 PM | Posted by sunday succi


Diamond Platnumz na kundi lake wakiwa na watoto yatima mjini Mombasa nchini Kenya walipotembelea makazi yao na kula chakula na watoto hao.
 
Diamond Platnumz akimsaidia mmoja ya watoto yatima wa kituo hicho mjini Mombasa nchini Kenya kula chakula.
Diamond Platnumz na kundi lake wakiwa kwenye kituo cha kulea watoto yatima mjini Mombasa nchini Kenya.
Diamond na kundi lake wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima mjini Mombasa nchini Kenya.

MIKATABA YA KIMATAIFA YAISAIDIA TANZANIA HIFADHI YA JAMII

Posted 2:08 PM | Posted by sunday succi


DSC_0382
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana (kulia) akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii unaotarajiwa kumalizika leo jijini Arusha. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi Wetu, Arusha
UTIAJI saini wa mikataba ya kimataifa, inayohusu hifadhi ya jamii kumeiwezesha Tanzania kuwa katika hatua nzuri ya kutekeleza ajenda yake ya kuhakikisha kwamba wananchi wake wanakuwa na haki sawa katika kujipatia maendeleo na ustawi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii mjini hapa.
Alisema mikataba mikubwa ya kimataifa ambayo Bunge la Tanzania limeridhia na iliyoleta mabadiliko makubwa katika sera na sheria nchini ni pamoja na Mkataba wa Kufuta Aina zote za Ubaguzi na Unyanyasaji kwa Wanawake (CEDAW) wa mwaka 1979, Mkataba wa Haki za Watoto (CRC) wa mwaka 1989 na Mkataba wa Afrika wa Haki za Watoto.
DSC_0394
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii unaomalizika leo jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van Berlekom.

Mikataba mingine ni Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MDGs), Azimio la Umoja wa Mataifa Namba 1325 la mwaka 2000 na Azimio Namba 1820 la 2006, ambayo inazungumzia ushiriki na uwezeshaji wa wanawake katika kutanzua migogoro na ujenzi wa taifa.
Alisema kitendo cha kuridhia kwa mikataba na maazimio hayo, kinaonesha ni kwa namna gani serikali ina utashi wa utekelezaji wa maazimio hayo kwa lengo la kuhakikisha watoto na wanawake, wanalindwa dhidi ya vurugu za aina zozote na kuwanyima haki zao za msingi.
Dk.Chana alisema kwa kuzingatia ushiriki kuleta katika maendeleo ya nchi, Tanzania imetayarishwa Dira ya Maendeleo ya 2025 ikiwa na vipengele vyote vya haki vyenye lengo la kuongeza wigo wa ushiriki wa wanawake.
Aidha, ili kuhakikisha makundi maalumu yanalindwa, serikali pia imetengeneza Sera ya Maendeleo ya Watoto ya mwaka 2008, ambayo kwa sasa inapitiwa ili kuingiza mambo mengine yanayohusu haki za mtoto.
DSC_0350
Picha juu na chini baadhi ya washiriki wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii wakiwemo watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania unaoendelea jijini Arusha.

Aidha, ikiwa imejikita kuondoa masuala ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia, serikali imefanya maamuzi mengi yenye manufaa pamoja na kushirikiana na wadau binafsi kuboresha maisha ya watanzania.
Alisema kwamba suala la wanawake na maendeleo, limeingizwa katika mkakati wa taifa wa kupunguza umaskini. Alisema mwaka jana serikali ilitengeneza programu ya taifa inayohusu wadau wengi ya miaka mitatu ya kuondokana na ukatili kwa watoto.
Mkutano huo unaozungumzia hifadhi, ulifunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ambaye alisema misingi imara imeshawekwa kusaidia hifadhi ya jamii kuelekea dira ya taifa ya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
DSC_0349

RUSHWA NI TATIZO SUGU KATIKA NCHI YETU, NANI ATAWEZA KUIONDOA?

Posted 2:06 PM | Posted by sunday succi

MWANDISHI Eric Shigongo
KATIKA kumuenzi Mungu, kila mtu ambaye leo afya yake ni nzuri hana budi kumshukuru na kumtukuza huku akimuomba awaponye wale wote walio katika magonjwa.

Baada ya kusema hayo nianze kwa kusema kuwa katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi, baadhi ya matawi wanachama wake wamelalamikia rushwa kwamba waliwapigia kura watu waliokuwa wanapenda kuwaongoza lakini kura zao zikachakachuliwa.

Nilisimuliwa kuhusu tawi moja eti waliochaguliwa waliiba kura na matokeo yakatajwa lakini baada ya msimamizi kupigwa na wanachama wenzake, kesho yake walioibiwa kura wakarudishiwa kura zao!
Wanachama hawakukubaliana na wizi huo na ikabidi sakata hilo lifikishwe ngazi ya wilaya.


Aliyeongoza katika uenyekiti akang’olewa lakini bado wanachama wanalalamikia wizi mkubwa uliofanyika katika kura za maoni kutokana na rushwa iliyotembezwa.

Hayo yametokea katika matawi mengi hapa nchini wakati wa kura za maoni. Hali hiyo si nzuri na inatoa changamoto mpya katika vita dhidi ya rushwa hasa kutokana na wananchi wengi kupoteza imani katika vita hiyo.

Wananchi ndiyo wanaoathirika moja kwa moja na rushwa na hawaoni hatua zozote madhubuti za kukomesha na kuwashughulikia watuhumiwa wa matukio hayo.Watanzania licha ya kuona matatizo hayo katika vyama vyao vya kisiasa, wamekuwa wakisumbuliwa na kulazimishwa kutoa rushwa wanapopata matatizo yanayohitaji huduma za kijamii hasa kwenye taasisi za umma ambazo zinaendeshwa na serikali kwa asilimia 100.

Watanzania pia wamekuwa wakiingia katika mtego wa kutoa rushwa baada ya kutembelea ofisi za serikali au watoa huduma katika sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali au ya dini katika maeneo yao.
Baadhi ya wananchi niliozungumza nao walisema waliwahi kuombwa rushwa na polisi, mahakimu au hata waliokuwa wakitafuta kazi.

Walisema polisi ndiyo wanaoongoza kwa kuomba rushwa.
Ukweli ni kwamba wananchi wamepoteza imani kabisa ya kupigana na rushwa kwa sababu hata zile kesi kubwa za rushwa zinazoibuliwa, mara nyingi zimekuwa zikipotelea hewani na hakuna anayewajibishwa.
Ni dhahiri hata Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) iliyopewa jukumu la kuchunguza, haijapewa meno ya kutosha.

Nashauri kwamba taasisi hiyo iwe na uwezo wa kusimamia uchunguzi na kuendesha kesi hizo yenyewe chini ya kiongozi wao Dk Edward Hosea.Kwa kutumia utafiti wa kipimo cha rushwa duniani wa 2013, uliofanywa na Shirika la Transparency International, Watanzania wamekuwa wakitoa rushwa mara nyingi zaidi kwa polisi.

Hata hivyo, wakati rushwa ikistawi nchini, Watanzania wengi hawana taarifa za kutosha na wengi hawajui kabisa kuhusu kashfa kubwa za rushwa zinazoelezwa katika vyombo vya habari.

Hili ni suala gumu lililoguswa katika ripoti ya utafiti huo na hadi matokeo yanatoka, asilimia zaidi ya 78 haikujua lolote kuhusu kashfa ya IPTL, asilimia 74 haijui lolote kuhusu kashfa ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati, David Jairo na asilimia 67 hawajui lolote kuhusu kashfa ya ununuzi wa rada.

Pia imegundulika kuwa asilimia 52 hawajui lolote kuhusu kashfa ya Epa na zaidi ya asilimia 44 hawajui lolote kuhusu kashfa ya Richmond.Wastani huo unashtua kwa sababu kwa idadi hiyo kubwa ya Watanzania wasiojua lolote kuhusu kashfa hizo kubwa za rushwa zinazowagusa moja kwa moja viongozi waandamizi serikalini, kunaonesha ni jinsi gani raia wasivyofuatilia mambo mazito.

Ukweli ni kwamba matatizo mengi ya nchi yanapata ‘kigugumizi’ katika kuyatatua hasa kashfa za rushwa kwa kuwa uelewa wa wananchi uko chini, licha ya kutangazwa na vyombo vya habari na kutawala mijadala ya kisiasa.

Katika utafiti huo, suala la rushwa katika sekta za usalama, siasa, kodi, ardhi, afya, elimu, maji, Serikali za Mitaa, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya dini, inawagusa zaidi ya asilimia 50 ambao wamefikia hatua ya kuiona kama ni kitu cha kawaida.

Wengi wamekuwa wakitoa rushwa wakiwa kwenye hali tete, hasa wanapokutana na polisi au wanapohitaji huduma za afya.Uombaji rushwa unaoshika nafasi ya pili ni ule unaowakabili wananchi wanapoomba ajira na sasa rushwa inatazamwa kama kitu cha kawaida kabisa.

Wakati wafadhili, wanasiasa na mashirika yasiyo ya kiserikali yakijikita kupambana na kashfa kubwa za rushwa, wananchi wengi wanaangalia zaidi aina ya rushwa inayowagusa moja kwa moja na kuathiri maisha yao ya kila siku.

Seriali chini ya Rais Jakaya Kikwete na wanasiasa wanaelekeza nguvu zao katika rushwa wanazoziita kubwa, ni sawa, lakini kutotilia maanani rushwa zinazowagusa wananchi moja kwa moja katika maisha yao ya kila siku katika huduma za polisi, afya, elimu na ardhi ni kosa kubwa. Kiongozi gani atakabiliana na tatizo hili?

Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli. GPL

BARABARA ZA JIJINI DAR KUENDELEA KUIMARISHWA

Posted 2:05 PM | Posted by sunday succi


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Mecki Sadiki akifungua mkutano wa Wajumbe wa Baodi ya Barabara ya Mkoa wea Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa Bi.Theresia Mmbando na Naibu Waziri wa Kazi Mh.Makongoro Mahanga (kulia).
Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam Muhandisi J. Nyamukama akiteta jambo na baadhi ya wahandisi wa ofisi yake leo jijini Dar es salaam wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara ya mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema(kushoto) na mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi wakifuatilia mkutano wa wajumbe wa Bodi ya barabara ya mkoa wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Ubungo Mh. John Myika akichangia kuhusu hali ya usafi na uimarishaji wa miundombinu katika jiji la Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya mkoa wa Dar es salaam Mh. Idd Azzan Mh. akichangia kuhusu hali ya usafi na uimarishaji wa miundombinu katika jiji la Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa

Waliokiuka makubaliano ya Ukawa kuwajibishwa

Posted 2:04 PM | Posted by sunday succi


Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyia Jumapili iliyopita. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa habari wa chama hicho, Abdul Kambaya. Picha na Rafael Lubava

Dar es Salaam. Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe amesema umoja huo utafanya tathmini ya maeneo ambayo wangeweza kushinda kwa kusimamisha mgombea mmoja kila eneo ili kuwachukulia hatua viongozi waliokiuka makubaliano hayo.
Wenyeviti wa umoja huo wa vyama vinne CUF, Chadema, NLD na NCCR Mageuzi, walisaini makubaliano kadhaa ikiwamo kusimamisha mgombea mmoja atakayeungwa mkono na Ukawa katika chaguzi zote kuanzia Serikali za Mitaa mpaka uchaguzi mkuu ujao.
Hata hivyo, katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Jumapili, katika baadhi ya maeneo, kila chama kilisimamisha mgombea wake na matokeo yake kuipa nafasi CCM kushinda.
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema alisema viongozi wote kutoka vyama hivyo waliohusika kukiuka makubaliano hayo watachukuliwa hatua za kinidhamu.
“Tutafanya tathmini ambayo itatupatia picha halisi ya sababu zilizochangia baadhi ya maeneo kukiuka makubaliano. Tutawachukulia hatua za kinidhamu. Tunajua hawakuwa na maandalizi na muda wenyewe ulikuwa hautoshi lakini tutaangalia kwa nini hali hiyo ilijitokeza,” alisema Mbowe.
Mbowe alisema awali, viongozi wa ngazi za juu katika umoja huo walitoa maagizo ambayo yalitakiwa kutekelezwa na wagombea wote wanaounda Ukawa.
“Hakuna mwanachama asiyejua kama umoja ni nguvu, kwa viongozi wa ngazi za juu tunalifahamu hilo kwa kiwango kikubwa lakini hata ngazi za chini wanatakiwa kulitambua hilo,” alisema.
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema changamoto hiyo imekuwa kikwazo ambacho kimesababisha kukosa ushindi katika maeneo mengi ya uchaguzi huo.
Nyambabe alisema tathmini itakayofanyika ndani ya umoja huo, itakuwa nafasi muhimu ya kujipanga kufanikiwa katika uchaguzi mkuu ujao.

ESCROW YAMNG'OA WAREMA

Posted 2:03 PM | Posted by sunday succi

  Kikwete amkubali kujiuzulu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, amejiuzulu.Jaji Werema amelazimika kujiuzulu kufuatia shinikizo kubwa kutoka kwa makundi kadhaa ya jamii na ushauri wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Rais Jakaya Kikwete, kutaka amfute kazi kutokana na kuhusishwa kwake na kashfa ya wizi wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ya Tegeta Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Jaji Werema alijiuzulu jana kupitia barua yake aliyomwandikia Rais Kikwete, akiomba kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo.Taarifa iliyotolewa jana usiku na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilisema:

“Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo (jana) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amekubali ombi hilo la kujiuzulu.”

Taarifa hiyo ilieleza kuwa katika barua yake kwa Rais Kikwete, Jaji Werema alisema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

“Mheshimiwa Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo fupi.Sakata la wizi wa fedha hizo liliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi, David Kafulila, katika mkutano wa Bunge la Bajeti mwaka huu, lakini serikali ilikanusha kuchotwa kwa fedha hizo kwa maelezo kuwa hazikuwa za umma.

Miongoni mwa viongozi waandamizi wa serikali waliotoa kauli za kupuuza hoja ya Kafulila ni Jaji Werema na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Jaji Werema alivutana na Kafulila kuhusiana na sakata hilo na kutoleana maneno makali, huku Jaji Werema akitishia kumpiga Kafulila, na ugomvi huo ulisuluhishwa na baadhi ya wabunge na mawaziri ndani ya Bungeni.

Kabla ya kutaka kumpiga, Jaji Werema alimuita Kafulila kuwa ni tumbili na Kafulila alijibu mapigo hayo kwa kumuita Jaji Werma kuwa ni mwizi.

Kutokana na shinikizo hilo, Waziri Mkuu alimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi katika akaunti hiyo na kuwasilisha taarifa hiyo bungeni.

Aidha, Waziri Mkuu aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza tuhuma hizo.

Katika mikutano ya Bunge ya 16 na 17 iliyomalizika Novemba 29, mwaka huu, wabunge walishinikiza serikali kuhakikisha kwamba ripoti ya CAG inawasilishwa bungeni na kujadiliwa.

Baada ya mvutano huo, ripoti hiyo iliwasilishwa katika Ofisi ya Spika na baadaye kukabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe.

Zitto na Makamu wake, Deo Filikunjombe waliwasilisha ripoti hiyo bungeni na kuzua mjadala mkubwa.

Kamati hiyo ilipendekeza baadhi ya vigogo kufutwa kazi wakiwamo Waziri Mkuu Pinda, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu, Eliakim Maswi; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.

WEREMA ALIVYOSHIRIKI ESCROW
Wakati PAC ilipokuwa imejichimbia Dodoma kuchambua ripoti ya uchunguzi ya CAG, kulikuwa na ushahidi ulioonyesha jinsi Werema na Maswi, walivyohusika kumuamuru Gavana wa BoT, Beno Ndulu, aidhinishe uchotaji wa fedha kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kwenda IPTL.

Akaunti hiyo ilikuwa imefunguliwa BoT ili kuhifadhi fedha zilizokuwa zinabishaniwa kati ya Tanesco na IPTL.

Jaji Werema alidaiwa kuandika barua Oktoba 2, mwaka 2013 yenye Kumbukumbu Namba AGCC/E.80/6/65 kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha (Hazina), Dk. Servacius Likwelile, akitaka fedha hizo zitolewe haraka.

Walioiona barua hiyo wanasema kuwa Jaji Werema aliinakili barua hiyo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Katika barua hiyo Jaji Werema alinukuliwa akibariki kuchotwa kwa fedha hizo kwa msingi wa maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu chini ya Jaji John Utamwa.

Habari zilieleza kuwa kwa mujibu wa barua ya Jaji Werema, maamuzi ya kuidhinisha kuchotwa kwa fedha hizo yanalindwa na maamuzi ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Utamwa.

Katika barua hiyo, Jaji Werema alinukuliwa akifafanua kwamba, aliisoma ripoti na kuwa suala ambalo lilioonekana kuishughulisha timu iliyohusika, ni uwekezaji wa fedha za Escrow.

Ilielezwa kuwa Jaji Werema alisisitiza kuwa Akaunti ya Escrow ilikuwa ni zao la makubaliano juu ya akaunti ya Tegeta Escrow yaliyofanyika Julai 5, 2006, huku akiirejea kuwa BoT kama wakala wa Escrow, iliruhusiwa kuziwekeza fedha hizo kwenye “uwekezaji ulioruhusiwa” kama inavyoelekezwa kwenye kifungu cha 3.4 na 7.2 (c) cha makubaliano hayo.

Ilielezwa kuwa Jaji Werema katika barua yake alisema, njia sahihi na ya busara ni kwa wakala wa Escrow kuijulisha IPTL kuhusiana na uwapo wa “uwekezaji ulioruhusiwa” na lini utaiva.

Jaji Werema alikwenda mbali na kusisitiza kuwa, hakuna pingamizi lolote kuhusu IPTL kupewa fedha hizo kwa sababu tayari kulikuwa na hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji Utamwa.

Alidaiwa kusema kuwa, uamuzi wa mahakama unalinda maslahi mapana ya umma dhidi ya malalamiko yasiyoisha juu ya fedha za akaunti ya Escrow.

Aidha, alidaiwa kusema kuwa ni maoni yake vile vile kwa wakala wa Escrow na serikali wazungumze na kukubaliana na IPTL juu ya nani anahusika na kukumbushia fedha hizo kabla hazijaiva kwa maslahi ya kampuni ili iendelee kufanya kazi.

Jaji Werema alinukuliwa akisema kuwa, udhamini wa serikali chini ya PPA ulikuwa umepitwa na wakati na kuonya kuwa serikali haiwezi kuwekwa kwenye hatari isiyotarajiwa kwa kuendelea kuhusika na fedha hizo.

Kadhalika, Jaji Werema alinukuliwa akipuuzia juu ya athari zinazoweza kutokea kutokana na kesi iliyofunguliwa na Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) dhidi ya wamiliki wa IPTL kuwa haitakuwa na madhara juu ya uamuzi wa kuhamisha fedha hizo kutoka Escrow kwenda IPTL na kama ni mashitaka mapya atakayeshtakiwa ni IPTL wala siyo Serikali ya Tanzania.

WEREMA NI NANI
Jaji werema aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo baada ya kustaafu kwa mtangulizi wake, Johnson Mwanyika mwaka 2010, alipata shahada ya kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1984. Mwaka 1993 alipata shahada ya pili ya sheria kutoka Washington DC, Marekani.

Wakili na Mkurugenzi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu mwaka 1984 hadi 2006.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania 2007-2009 Kung’oka kwa Werema kunawaachia mtihani wateule wengine wa Rais waliotajwa katika kashfa hiyo, Prof. Muhongo na Maswi pamoja na Profesa Tibaijuka ambaye alitajwa kupata mgawo wa Sh. bilioni 1.6 kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engneering Limited, James Rugemalira. VIP ilikuwa mwanahisa katika IPTL.

Ikulu Desemba 9, mwaka huu, ilitoa taarifa ikieleza kwamba Rais Kikwete atafanya maamuzi kuhusiana na sakata la Escrow wiki hii.

MHE. HAWA GHASIA ASEMA HAJIUZULU NG'O KUFUATIA KASHFA YA KUVURUGIKA KWA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Posted 2:01 PM | Posted by sunday succiWaziri wanchi ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema leo Jumatano Desemba 17, 2014, kuwa hatajiuzulu ng’o kutoka wadhifa wake, kufuatia kashfa ya kuvurugika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini Jumapili iliyopita. Badala yake, waziri Ghasia amesema wakurugenzi watano wamefutwa kazi, huku wenghine kadhaa wamesimamishwa na wengine kushushwa vyeo. 
Waziri Ghasia, akitoka kwenye cnhumba cha mkutano na waandishi wa habafri mara baada ya kuzungumza nao
Waziri Ghasia na katibu mkuu wa TAMISEMI, Jumanne Sagini
Tangazo la waziri Ghasia alilotoa leo Jumatano Desemba 17, 2014, kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam
Wakurugenzi watano wamesimamishwa kwazi

IDARA YA UHAMIAJI MKOA WA NJOMBE YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA WILAYANI MAKETE

Posted 2:00 PM | Posted by sunday succi


Watoto yatima wakipewa zawadi na Idara ya uhamiaji mkoa wa Njombe
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akiwa amembeba mtoto yatima anayelelewa kituo cha Nyumba ya yatima Bulongwa
Baadhi ya msaada uliotolewa
Mkuu wa wilaya akikabidhiwa msaada huo na afisa uhamiaji mkoa wa Njombe.

Hivi karibuni Idara ya uhamiaji mkoa wa Njombe iliunga mkono jitihada za mkuu wa wilaya ya makete Josephine Matiro kusaidia vituo vya watoto yatima wilayani humo kwa kutoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 1

Akizungumza wakati akikabidhi msaada wao afisa uhamiaji mkoa wa Njombe Rose Mhagama alisema wameguswa na suala hilo na kuamua kuvisaidia vituo vya watoto yatima Makete vitu mbalimbali, na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia watoto hao

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Hiyo Bi Josephine matiro amewataka wanamakete kubadilika na kuacha dhana kuwa watoto hao watasaidiwa na wafadhili kutoka nje na badala yake nao wawasaidie watoto hao kwa kitu chochote walichojaliwa na Mungu

Vituo vilivyonufaika ni Nyumba ya yatima Bulongwa, Fema Matamba na Kituo kipya cha Kisinga

ESCROW: Mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Werema ajiuzulu

Posted 1:58 PM | Posted by sunday succi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema (pichani) leo amejiuzulu nafasi yake na tayari amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Kikwete.
Rais Kikwete asema amepokea barua yake na kumshukuru kwa ushirikiano aliouonyesha katika kipindi chote cha utumishi wake.

Sababu ya kujiuzulu ni kwamba ushauri alioutoa kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka vizuri.

D'BANJ AMZAWADIA RAIS WAKE WA NIGERIA ZAWADI HII YA CHRISTMAS

Posted 1:54 PM | Posted by sunday succi

Beats By Dre
Dapo Daniel Oyebanjo a.k.a D’Banj amekuwa Balozi wa bidhaa za Beats by Dre kwa upande wa Afrika kwa miezi kadhaa sasa, dili linalomfanya aongeze ile mirija ya kujaza akaunti zake za Benki Naira nyingi tu kila mwezi.
Beats by Dre zina heshima yake kubwa sokoni kwa sasa, najua unajua hilo, kingine ni kwamba kuna zile special ambazo huwa zinatengenezwa chache na maalum kabisa, mtu ambaye anaweza kupewa labda ni Balozi wao au mtu mwingine maalum kama zawadi, kama ikitokea zikiuzwa basi bei yake huwa ni bei maalum vilevile.
Katika zile special ambazo zimewahi kutolewa kwa Balozi D’Banj, aliwahi kumpa zawadi ya aina hiyo Iyanya wakiwa Airport Nigeria, baada ya hizo taarifa ikufikie kwamba safari hii zali hilo limemuangukia Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan.
Kaweka picha Instagram (iambangalee) akimvalisha Mr. President mzigo huo, mitandao ya Naija haikukosa neno, wanasema eti Rais alionekana kama hakuipokea poa hii ya kuvalishwa headphone hizo, huenda Balozi huyo alikiuka protocol labda.
Aliandika hivi kwenye post hiyo; “Merry Christmas Mr President with Love from@iambangalee and @Beatsbydre OooSssHhhEee“– @iambangalee
Cheki tukio zima hapa.
DBanj-600x600
17-564x372
DBanj1-600x600

MAPACHA WALIOUNGANA WATENGANISHWA

Posted 1:51 PM | Posted by sunday succi


Watanzania waendelea kufaidika kutoka kwa hospitali ya Apollo iliyoko nchini India. Hii ni kufuatia hosiptali hiyo kufanikiwa kuwatenganisha mapacha wa kike Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na tumboni kutoka nchini Tanzania katika upasuaji uliofanyika tarehe 17 Novemba 2014 nchini India. Mapacha waliounganika kwa mtindo huu hujulikana kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.

Mapacha Abriana na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya kifua na tumbo, hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo na maini yaliyounganika. Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa kwa madaktari ulikuwa kufanya utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi ambayo waliweza kukabiliana nayo ipasavyo kutokana na madaktari waliokuwepo wenye wataalum wa kiufundi na matibabu.

Upasuaji huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbali mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa masaa 11. Watalaamu walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyo kuwa vimeungana lakini mapacha hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo kusaidia zoezi zima la uponyaji baada ya upasuaji.

Hali kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa kurudisha viungi husika katika mahala pake baada ya kuvitenganisha. Akizungumzia kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive Surgeon anasema, “Baada ya upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa nne kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahala pake.”

Upasuaji huu wa mafanikio wa mapacha waliounganika kutoka ncini Tanzania sio wa kwanza kufanywa na hospitali ya Apollo. Mwishoni mwa mwaka 2013 mapacha wengine wakiume waliokuwa wameungana na kujulikana na wataalamu kama Pygopagus, Ericana & Eluidi kutoka Tanzania walifanikiwa kutenganishwa na wataalamu wa hospitali hiyo. Matukio amabayo yamepandisha chati na kuipa hadhi ya juu hospitali ya Apollo iliyoko nchini India na nchi ya India kwa ujumla kama kiongozi katika sekta ya afya na mfano wa kuigwa na nchi nyingine ikiwemo Tanzania. Hospitali hiyo ina mahusiano mazuri na nchi ya Tanzania ikitembelewa idadi kubwa ya wagonjwa kutoka Tanzania kutokana na ukosefu wa huduma muhimu na za kisasa nchini.

Wapacha walioungana hutambuliwa na kupewa majina kutokana na jinsi muungano huo unapokuwa katika viungo mbali mbali vya mwili. Ikiwa aina ya mapacha waliounganika wa Thoraco Omphalopagus ndio inayoongoza kuripotiwa kwa asilimia 28% zaidi ya aina nyingine zote zinazotambulika matukio mengi yakitokea zaidi Kusini-Magharibi mwa bara la Asia, Africa and Brazili. Katika aina hii mapacha wanakuwa wameunganika kuaznia kifuani mpaka chini ya kifua kwenda kwenye tumbo na hutumia baadhi ya sehemu ya moyo, ini na baadhi ya sehemu viungo vya mmeng’enyo wa chakula(i).

Kulingana na hospitali ya Apollo kesi zinazohusu mapacha waliounganika huwa ni nadra mathalan moja kati ya uzao 200,000 huonekana. Lakini, asilimia 60 ya hao hufariki wakati asilimia 35 hufariki katika kipindi kifupi baada ya kuzaliwa kutokana na sababu mbali mbali (ii).

Akizungumzia upasuaji huo uliokuwa na mafanikio, Dkt. Prathap C Reddy, Mwenyekiti na Muanzilishi wa Hospitali za Apollo anasema, “Nikitazama katika mwaka huu wa 2014 naona maisha ya watu tuliweza kuyagusa kwa namna njema. Mbali na maumivu wanayopata watoto yatokanayo na ugonjwa, wazazi pia hupitia mshituko na mahangaiko makubwa. Nchi nyingi za bara la Afrika zinakosa tiba muhimu na mbadala na hivyo kujikuta wanakuja nchini India kupata huduma hizo muhimu na kisasa. Inafurahisha na kuleta faraja kuwa katika sikukuu hii ya Krismasi Jimmy na Carolyn watarudi nyumbani na watoto wao wakiwa ni binadamu wawili tofauti.”


Tangu mwaka 2007, jozi nane za mapacha waliounganika katika ini na utumbo kutoka sehemu mbali mbali nchini India zimeripotiwa kutenganishwa. Aradhana na Stuthi ni jozi pekee ya mapacha waliwahi kutenganishwa kwa upasuaji wakiwa na mioyo iliyo katika mvungu (cavity) mmoja hali sawa na mapacha Adrianan na Abriana. Japo moja ya mapacha wa thoraco opmhalopagus Aradhana kufariki wiki tatu baadae, Adriana and Abriana na ndio aina hiyo ya mapacha walioweza kuishi baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa.

Baada ya miezi ya matibabu, mapacha Adriana na Abriana kutoka Dar-es-Salaam watarejea nyumbani Tanzania tarehe 18 Disemba na kufika mjini Dar es Saaam asubuhi ya tarehe 19 Disemba. Katika kipindi hiki cha sikukuu itakuwa shangwe kwa wazazi Jimmy na Carolyn wanaporudi nyumbani kutoka nchini India wakiwa na watoto wao wawili waliotenganishwa.