MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia huru mwanamuziki Rashid Makwilo
'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 au kwenda jela miaka
miwili kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya, ambapo
amefanikiwaa kulipa pesa hizo na kuachiwa huru.
Chid
Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo
misokoto ya bangi.
Chidi Benz alikiri kosa hilo wiki iliyopita, mbele ya mahakama ya kisutu
kuwa alikamatwa uwanjani hapo na madawa ya kulevya yenye thamani ya
shilingi 38,000 na bangi yenye thamani ya ashilingi 1,700, pamoja na
vifaa vya kuvutia ambavyo ni kigae na kijiko, akiwa anajitayarisha
kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.
akizungumza na Clouds Fm ndani ya xxl live leo hii, Chidi amesema:
"Nimejifunza kwasababu kuna maisha halisi ambayo mimi nimeyaishi kati
kati hapo, matatizo na kwenye maisha mi naona yamebadilisha sehem kubwa
sana ya mimi mwenyewe ninavyoishi. Tukio la kwanza ambalo watu wote
wanafahamu kwamba huyu jamaa lilimtokea na amelimaliza na amemalizana
nalo na kila mtu analiona na analifatilia. Mimejifunza mengi sana katika
hili tangu lilivyotokea, nashkuru," amesema Chidi Benz
0 comments:
Post a Comment