Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi
Chana (kulia) akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa
unaohusu hifadhi ya jamii unaotarajiwa kumalizika leo jijini Arusha.
Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe
Stephen Kebwe na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Pereira Ame Silima.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi Wetu, Arusha
UTIAJI saini wa mikataba ya kimataifa,
inayohusu hifadhi ya jamii kumeiwezesha Tanzania kuwa katika hatua nzuri
ya kutekeleza ajenda yake ya kuhakikisha kwamba wananchi wake wanakuwa
na haki sawa katika kujipatia maendeleo na ustawi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana katika mkutano wa
siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii mjini hapa.
Alisema mikataba mikubwa ya kimataifa ambayo
Bunge la Tanzania limeridhia na iliyoleta mabadiliko makubwa katika
sera na sheria nchini ni pamoja na Mkataba wa Kufuta Aina zote za
Ubaguzi na Unyanyasaji kwa Wanawake (CEDAW) wa mwaka 1979, Mkataba wa
Haki za Watoto (CRC) wa mwaka 1989 na Mkataba wa Afrika wa Haki za
Watoto.
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka
makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano
mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya
Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la
kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu
katika jamii unaomalizika leo jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Mkuu wa
Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini,
Maria Van Berlekom.
Mikataba mingine ni Mpango wa Maendeleo wa
Milenia (MDGs), Azimio la Umoja wa Mataifa Namba 1325 la mwaka 2000 na
Azimio Namba 1820 la 2006, ambayo inazungumzia ushiriki na uwezeshaji
wa wanawake katika kutanzua migogoro na ujenzi wa taifa.
Alisema kitendo cha kuridhia kwa mikataba na
maazimio hayo, kinaonesha ni kwa namna gani serikali ina utashi wa
utekelezaji wa maazimio hayo kwa lengo la kuhakikisha watoto na
wanawake, wanalindwa dhidi ya vurugu za aina zozote na kuwanyima haki
zao za msingi.
Dk.Chana alisema kwa kuzingatia ushiriki
kuleta katika maendeleo ya nchi, Tanzania imetayarishwa Dira ya
Maendeleo ya 2025 ikiwa na vipengele vyote vya haki vyenye lengo la
kuongeza wigo wa ushiriki wa wanawake.
Aidha, ili kuhakikisha makundi maalumu
yanalindwa, serikali pia imetengeneza Sera ya Maendeleo ya Watoto ya
mwaka 2008, ambayo kwa sasa inapitiwa ili kuingiza mambo mengine
yanayohusu haki za mtoto.
Picha juu na chini baadhi ya washiriki wa mkutano mkubwa wa
kimataifa wa hifadhi ya jamii wakiwemo watengeneza sera, watafiti na
waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda,
Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia,
Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania unaoendelea jijini Arusha.
Aidha, ikiwa imejikita kuondoa masuala ya
kuondoa udhalilishaji wa kijinsia, serikali imefanya maamuzi mengi yenye
manufaa pamoja na kushirikiana na wadau binafsi kuboresha maisha ya
watanzania.
Alisema kwamba suala la wanawake na
maendeleo, limeingizwa katika mkakati wa taifa wa kupunguza umaskini.
Alisema mwaka jana serikali ilitengeneza programu ya taifa inayohusu
wadau wengi ya miaka mitatu ya kuondokana na ukatili kwa watoto.
Mkutano huo unaozungumzia hifadhi,
ulifunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi
ambaye alisema misingi imara imeshawekwa kusaidia hifadhi ya jamii
kuelekea dira ya taifa ya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
0 comments:
Post a Comment