Indira, alikuwa binti wa Jawaharlal Nehru,
aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza India kati ya 1947 hadi 1964, naye
aliweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke India.
Ukoo wa Jawaharlal Nehru una historia ndefu katika siasa za India, kutokana na ndugu wengi kushiriki siasa.
Hata baba yake Rajiv, Feroze alikuwa mwanachama wa
Chama cha Indian National Congress. Bibi yake Rajiv, Kamala Nehru naye
alikuwa mwanachama wa chama cha Allahabad.
Feroze na Indira walikuwa marafiki wa karibu
wakati wanasoma Uingereza kabla ya kuja kuoana na kupata watoto wawili,
Rajiv na Sanjay.
Rajiv aliuawa Agosti 20, 1944 kwa bomu la kujitoa
muhanga Mei 21, 1991 wakati akiwa kwenye kampeni za uchaguzi. Mama yake
pia (Indira) aliuawa kwa na walinzi wake.
Mwanzoni, Gandhi hakuwahi kuonekana kama mshirika wa mambo ya siasa, kwani fani yake kubwa ilikuwa urubani wa ndege.
Mwaka 1966, alirejea India baada ya kumaliza
masomo ya urubani na kuajiriwa Shirika la Ndege la India. Mwaka 1968
alimuoa Antonia Maino, mwanamama aliyeanza naye uhusiano wakati akisoma
Uingereza.
Baada ya kufunga ndoa, Maino alibadilisha jina na
kuwa Sonia Gandhi. Rajiv alianza kujiingiza kwenye siasa kutokana na
ushawishi wa mama yake baada ya kufariki ndugu yake Sanjay, aliyependa
mambo ya siasa.
Rajiv alitangazwa kuwa Waziri Mkuu wa India saa
chache baada ya mama yake aliyekuwa akishika cheo hicho, Indira Gandhi
kuuawa Oktoba 31, mwaka 1984.
Utawala wa Rajiv ulianza kukumbwa na misukosuko
siku chache baada ya kuapishwa baada ya kutokea vurugu zilizosababisha
mamia ya watu kuuawa katika maandamano ya kuipinga jamii ya watu wa
Sikh.
Katika kipindi chote cha utawala wake, Rajiv
aliyekuwa Rais wa Chama cha Congress hakuwahi kuwa mbali na misukosuko
hali iliyomfanya kutengeneza maadui wengi.
0 comments:
Post a Comment