Wakati huu ambapo kumekua na stori zilizoenea mtaani kuhusu yeye na ndoa yake pia kazi, show ya TV ya Mkasi inayoongozwa na mtangazaji Salama Jabir imepata nafasi Exclusive ya kuongea nae.
Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya sentensi alizoziongea Captain G kwenye Mkasi on EATV.
- Kwanza alianza kwa kuongelea jinsi alivyoingia kufanya kazi Redioni huku akimkumbuka Othman Njaidi aliemchukua na kumpeleka CloudsFM sio kama mtangazaji bali akajiunge na timu ya Marketing, akakutanishwa na Ruge Mutahaba aliekua General Manager wakati huo ambae alipoisikia tu lafudhi ya Gardner akasema huyu anafaa kuwa mtangazaji.
-
Staa aliefurahi baada ya kukutana nae ni D’Banj wa Nigeria, alifurahia uchangamfu wake…
-
Salama alipomuuliza kuhusu uhodari wake wa kutangaza habari za mastaa
wa dunia… Captain G. akasema ‘nilikua nanunua majarida kwenye maduka
yanayouza majarida kutoka nje, wakati Internet hamna kulikua na majarida
mengi kidogo’
-
‘Mimi ni mchaga kabisa wa Baba na Mama lakini Wazazi wangu walihamia
Tanga zamani alafu mimi nimezaliwa Ngamiani pale Hospitali na tukaishi
Chumbageni muda mrefu kwa hiyo nilipata lafudhi ya Tanga pale, na
hiyohiyo lafudhi ya Tanga ndio iliyonipa kazi kwenye Radio’
-
Salama akamuuliza ‘Unajisikiaje ukisikia mtu anatangaza kama wewe‘
>> Gardner akajibu ‘kuna baadhi ya watu kusema ukweli
wanachukizwa sana na hicho kitu na wananilalamikia sana kwamba kuna
Watangazaji wengi wamekua wanakuiga kwenye kutangaza Redioni na kwenye
kutengeneza jingle kama za kwako lakini mimi nimeiona ni baraka kwangu,
kama watu wamekupenda kiasi kwamba wanakuiga ni jambo la kufurahisha
kwangu mimi linanifurahisha sana’
-
Kuhusu kitu kilichomfanya akaondoka kwenye Radio, Captain amesema
‘Nilifanya kazi miaka 9 akili ikawa imechoka nikafikiria lazima pia
nifanye biashara watu wanakusifia kwamba una uhodari flani kwa hiyo
unajipa challenge kwanini nisitengeneze kitu changu, ndio tukafungua
biashara za chakula lakini zaidi nilikua nataka kupumzika’
-
Swali jingine kutoka kwa Salama likawa ‘nasikia kuna stori kwamba hivi karibuni pia unaweza kurudi kule ama ukaenda sehemu nyingine‘
Captain G. akajibu >>> ‘ni mmoja kati ya hao wawili, stori ni
ya ukweli ndio maana naondoka, nimemaliza mkataba nimepata ofa nyingine
kubwa naichukua’
-
Swali jingine lililokua linasubiriwa ni hili alilouliza Salama
>> ‘kuna stori mtaani kwamba wewe na Lady Jaydee mmeachana’
Gardner akajibu ‘mimi sijawahi kupata interview muda mrefu sana… nadhani
hii inaweza kuwa interview yangu ya kwanza, kwahiyo nilikua nataka
nikuombe tuongee kuhusu mimi kwanza manake tukizungumzia kuhusu JayDee
nitafunikwa hapa’
0 comments:
Post a Comment