
Movie
mpya ya Angelina Jolie ( Maleficent) ni movie ambayo siku inaonyeshwa
kwa mara ya kwanza wiki iliyopita kulitokea ishu ya Brad Pitt ambae ni
mume wa Angelina Jolie kuvamiwa na kupigwa usoni na mtu yuleyule ambae
amekua akihusishwa kuvamia mastaa kwenye red carpet kama Will Smith.

Angelina kwenye movie yake mpya ya Maleficent
Brad hakuumia na badala yake aliendelea kukutana na mashabiki
mbalimbali waliojitokeza huku aliemvamia akikamatwa na kupelekwa polisi
ambapo taarifa mpya kuhusu huyu jamaa aliemshambulia Brad, ni kwamba
atakua chini ya uangalizi kwa miaka mitatu na pia ameonywa kuwa
anatakiwa kukaa mbali na shughuli za mastaa kwa umbali wa mita 457.
Show ambazo hatakiwi kujisogeza ni pamoja na uonyeshwaji wa movie
pamoja na utolewaji wa tuzo na pia katika uangalizi wa miaka mitatu,
Sediuk anatakiwa kufanya kazi za kijamii kwa siku 20.

Sediuk
pia ameonywa kukaa mbali kabisa na Angelina Jolie pamoja na Brad,
vilevile atatakiwa kwenda kupata ushauri kutoka kwa wataalamu
Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.
0 comments:
Post a Comment