Jamaa aliyeigiza kama Idi Amini amefariki Dunia.

TZA JOSEPH OLITA -IDI AMIN.2Wakati Tanzania tukiendelea kuwa na majozi ya vifo 3 mfululizo kutoka kwenye tasnia ya filamu Tanzania,wenzetu nao Uganda wamempoteza jamaa aliyeigiza kama Idi Amini,Idi Amini wengi wanamfahamu kutokana na matukio mengi aliyowahi kufanya ingawa kuna kizazi hakikuwahi kumuona.
Kupitia filamu ya  The Rise and Fall of Idi Amin,jamaa alicheza kama Idi Amini  na filamu hii ilikua ikielezea matukio yote aliyowahi kuyafanya Idi Amini enzi za uhai wake.
Joseph Olita ambaye ndiye aliyecheza kama Idi Amini amefariki jumapili ya June 01 akiwa na umri wa miaka 70 kusini mashariki mwa Alego huko kogelo Nchini Kenya na ilikua baada ya kumaliza mazishi ya mama yake mzazi.
TZA JOSEPH OLITA -IDI AMINMmoja wa ndugu wa Joseph,Bi.Risper Odero amesema kifo cha Joseph Olita kimetokana na shinikizo la damu iliyosababishwa na shughuli nyingi na majonzi wakati wa kumuaga marehemu mama yake mzazi.
Bi Odero amesema kifo cha Olita ni pigo kwa familia hiyo hasa baada ya kumuaga mama yao mzazi masaa kadha kabla ya kifo cha olita,Olita alikua anafanana sana na aliyekua kiongozi wa kiimla Uganda bwana Idi Amin Dada.
Miongoni mwa vitu walivyokuwa wanafanana ni pamoja urefu wa futi sita nchi 5.5 na uzito wa kilogramu 150 na ndiyo maumbile pekee yaliyo wafanya wengi kudhani kuwa olita alikua ndiye Idi Amin.
Mbali na filamu ya The Rise and Fall of Idi Amin ya miaka ya 80 iliyobeba maisha ya Idi Amin kama kiongozi wa kimila aliyeingia madarakani mwaka wa 1971 na kutolewa mwaka 1979 pia ameigiza kwenye filamu ya Mississippi Masala mwaka 1991 na amewahi kuigiza kama polisi kwenye filamu ya Sheena ya mwaka 1984.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment