Kundi maarufu kwenye muziki wa Hiphop linalojumuisha wasanii kama 50 Cent,Llyoid Banks,Young Buck na Tony Yeyo waliwahi kutamba sana kwenye muziki wakiwa kama kundi na solo artist.
Baada ya muda waligawanyika baada ya msanii Young Buck kujitoa na hata utawala wao kwenye muziki ukapungua. Hivi sasa 50 cent amepost picha ikidokeza kwamba kundi hilo limeungana tena kama zamani.
Picha hiyo inawaonyesha wasanii hao wanne wakiwa kwenye pamoja na 50 cent aliandika, “Things go the way I say they go.now I think it’s time we get busy”.
Kwenye comment ya picha hiyo mashabiki wengi wameonekana kufurahia kuungana tena kwa kundi hilo, hii ni moja nyimbo zilizowahi kufanya vizuri enzi zao wakiwa pamoja.
0 comments:
Post a Comment