Ripota
wa SUCCI1 nchini Kenya Julius Kepkoitch anaripoti kwamba baada ya kikundi
cha kigaidi cha Al Shabaab cha Somalia kutoa onyo kwamba mashambulizi
yake yanayofata yatawahusu viongozi wa Kenya, imebidi system ya ulinzi
wa rais kwenye msafara ibadilike.
Unaambiwa mabadiliko yalianza kuonekana toka mwishoni mwa wiki
iliyopita kwenye sherehe za 51 za kujitawala ambapo badala ya Rais
kutumia gari aina ya Land rover iliyo wazi iliyokua pia ikitumika na
marais wa awali, rais aliiingia kwenye uwanja wa michezo wa nyayo na
gari aina ya Land cruiser iliyo na vioo visivyo penya risasi.
Hiyo
Land Cruiser ililoongozwa na gari lenye mitambo iliyo na uwezo wa
kugundua bomu kwa zaidi ya kilomita 10, nyuma kabisa kulikua na gari
lililo na uwezo wa kuhimili risasi na bomu au kilipuzi cha aina yoyote
na inasemekana kwamba gari hilo huwa linatumika endapo msafara wa Rais
umeshambuliwa kwa haraka Rais na wakuu wengine wanaondolewa na gari
hilo.
Home
imebidi msafara wa rais uwe hivi
Yani baada ya Al Shabaab kusema wataua viongozi Kenya
Yani baada ya Al Shabaab kusema wataua viongozi Kenya, imebidi msafara wa rais uwe hivi
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment