Watalamu hao waliohitimu kutoka Chuo Kikuu cha
Kilimo Sokoine (SUA) pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
wamefanya kazi kwa kipindi kisichozidi miezi sita kabla ya ajira zao
kusitishwa.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa kikao cha
kusitisha ajira za vijana hao kilifanyika Januari, kati ya wizara na
wawakilishi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Serikali ilieleza wataalamu hao hawana sifa za
kisheria za kuwawezesha kusajiliwa au kupata leseni ya Baraza la
Wataalamu wa Maabara wa Afya nchini, bali wanatambulika kwa uwezo wao wa
kufanya utafiti wa kisayansi katika maeneo husika.
Baada ya kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu wa wizara
hiyo, Dk Donan Mmbando alitoa agizo kwa waajiri wote nchini ambao ni
makatibu wakuu, makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri
za jiji, manispaa na wilaya kote Tanzania Bara kufuta ajira hizo za
maofisa wa teknolojia Daraja la II.
“Kwa mujibu wa waraka huu, wanaostahili kuajiriwa
kama wateknolojia daraja la II ni wenye shahada ya sayansi katika
mojawapo ya fani za maabara, radiolojia, macho, viungo bandia, meno na
dawa kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na mabaraza
ya taaluma,” inaeleza sehemu ya waraka hiyo ya Dk Mmbando.
Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja,
alisema kuwa hakuna mabadiliko yoyote yanayoweza kufanywa baada ya
maamuzi yaliyofikiwa na kikao cha Januari.
Wataalamu
Profesa Joshua Malago kutoka Sua anasema kuwa
katika kikao hicho ilibainika kuwa kuna kozi mbili ambazo hazifundishwi
katika vyuo hivi viwili na kwamba ndivyo vilivyowanyima wahitimu wao
leseni kutoka bodi husika.
“Elimu ya wahitimu wetu iko juu sana kuliko hata
wanaozalishwa katika vyuo vingine wanavyovitambua, changamoto pekee ni
‘patient handling na anatomy’. Lakini tumekubaliana tuziongeze. Ni kozi
rahisi kuliko ambazo tumewafundisha na zinaweza zikafundishwa ndani ya
wiki mbili au tatu kama utaratibu utaandaliwa wa kuwapa ‘on job
training,” anasema Profesa Malago.
Malago anaongeza kuwa taarifa walizozipata kutoka
kwa wahitimu wao waliokuja kujiendeleza wakiwa wametoka kazini zinaeleza
kuwa hawajakubaliwa na bodi za taaluma zao kusajiri vyeti vyao vya
shahada.
“Wanatambulika kuwa na stashahada hata baada ya kupata shahada yetu ambayo inatambulika kimataifa,” anaeleza Profesa Malago.
0 comments:
Post a Comment