Madini ni vitu ambavyo vina thamani, hivyo kama yanasimamiwa vizuri yanakuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi.
Tanzania inatajwa kama nchi ya nne barani Afrika
kwa kuzalisha madini kwa ujumla na ya tatu nyuma ya Afrika Kusini na
Ghana kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu. Madini mengine yanayochimbwa
nchini ni pamoja na almasi, rubi, tanzanite na ulanga.
Katika uzalishaji huo, kuna baadhi ya migodi
inamilikiwa na wachimbaji wadogo wazalendo na mingine inamilikiwa na
wachimbaji wakubwa hususani makampuni ya kigeni na mingine inamilikiwa
kwa ubia baina ya wageni na wazawa.
Serikali pia ina hisa katika baadhi ya migodi ya madini kupitia Shirika la Shirika la Madini la Taifa (Stamico).
Kupitia madini, mbali ya faida kama vile kutoa
ajira kwa wananchi na kutoa bidhaa za kutumika migodini, pia Serikali
inastahili kupata fedha nyingi kama mrabaha, na malipo ya kodi.
Mirabaha na kodi hizi hulipwa kwa mujibu wa sheria na mikataba iliyofikiwa baina ya Serikali na kampuni za uchimbaji madini.
Sheria na mikataba inapokuwa mizuri huipatia
Serikali mapato makubwa, lakini sheria dhaifu na mikataba mibovu
huipotezea nchi kipato, matokeo yake ni Taifa na wananchi wake kwa
ujumla kuendelea kuwa duni kiuchumi licha ya kuwa na madini mengi.
Nguvu ya mikataba ya madini
Kwa mujibu wa sheria inayotumika ambayo ni Sheria
ya Madini ya Mwaka 2010 na.14, ambayo ndiyo inayowaongoza kuhusu
uchimbaji, utafutaji na usafirishaji wa madini, kimsingi mkataba wa
madini unaingiwa kati ya mwekezaji kwa upande mmoja na waziri wa madini
kwa upande mwingine. Waziri huyo huingia mkataba husika kwa niaba ya
Watanzania wote.
Sheria imeweka mfano wa mkataba huo (sample agreement) chini ya tangazo la gazeti la Serikali na. 405 la tarehe 5/11/2010.
Kanuni ya 19 ya tangazo hilo inaruhusu Serikali
kuboresha mfano huo wa mkataba kwa kuongeza vifungu au kifungu chochote
wanachoona kinafaa.
0 comments:
Post a Comment