“Alinikataza kulia kwa sauti na kunitisha kuwa ataniua au kuniroga nikimwambia mtu yeyote yale aliyokuwa ananifanyia.”
Yusta anasema kuwa tajiri yake huyo alibadilika
zaidi baada ya kuondoka kwa mumewe ambaye hajui kama waliachana au
alihama kikazi.
“Mwaka 2012 mumewe aliondoka na hapo ndipo
matatizo yalizidi kwani hata mwanaye ambaye yuko kidato cha tatu
alimpeleka shule ya bweni hivyo tulibaki wawili tu na hakukuwa na mtu wa
kunisaidia,” anasema.
“Alinining’ata kila sehemu katika mwili wangu na
alipoona damu imejaa mdomoni alitema na kisha kuendelea kuning’ata mpaka
pale aliporidhika. Wakati mwingine alining’ata hadi usoni.”
Alisema alimfungia geti na kuondoka na funguo kila
alipotoka kwenda kazini na alipomtuma sokoni alimuamuru kwenda haraka
na kumkataza kuzungumza na mtu yoyote njiani hata majirani.
Aliongeza baada ya kuondoka kwa muwewe, Amina
alikuwa na kawaida ya kwenda kwa waganga wa kienyeji na wakati mwingine
waganga hao walifika nyumbani na kila walipofika alimfukuza na kumfungia
chumbani hivyo hakujua walikuwa wakifanya nini.
Alitokaje kwenye kifungo
Usiku wa Kuamkia Alhamisi ya Juni 5, binti huyo
alifanikiwa kutoka katika ‘kifungo’. Majirani wa Amina ambao walishidwa
kuendelea kuvumilia kusikia sauti za kilio cha Yusta mara kwa mara hasa
nyakati za usiku.
Majirani hao waliamua kupeleka taarifa za jambo
hilo kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya Jipange ambayo inafanya shughuli
za kutetea wanawake. Baada ya kupata taarifa hizo, Jipange walitoa
taarifa polisi na hapo ndipo mtego wa kumnasa Amina uliwekwa na hatimaye
majira ya saa 8:00 usiku alikamatwa akiwa katika harakati za kukimbia
na kumtorosha Yusta ili kuficha ushahidi.
Mwenyekiti wa Jipange, Janet Mawinza alisema
walipopata taarifa za Yusta kutoka kwa wasamaria wema, waliwashirikisha
polisi, lakini kwa bahati mbaya taarifa zilivuja na kumfikia mtuhumiwa
hivyo alipanga njia ya kutoroka.
“Tulifika nyumbani kwa Amina majira ya usiku ili
kulinda mtu asitoke, lakini kumbe yeye alishafahamu ujio wetu, hivyo
aliruka dirisha na kukimbia. Alimkabidhi Yusta kwa kijana
aliyetayarishwa kumtorosha.”
0 comments:
Post a Comment