Sakata
la Michael Wambura kuondolewa kwenye kinyang’anyiro za uchaguzi wa mkuu
wa Uraisi wa klabu ya Simba SC leo limefikia tamati.
Kamati ya rufani ya shirikisho la soka
Tanzania, TFF, imetengeu maamuzi ya kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba
SC wa kuliengua jina la mgombea wa Urais wa klabu hiyo, Micheal Richard
Wambura.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, wakili Julius
Mutabazi Lugaziya amesema mchana huu katika mkutano na waandishi wa
habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF, jijini Dar es salaam kuwa
kamati yake ilikaa juzi na jana na kufikia maamuzi ya kutengua maamuzi
ya kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya mwanasheria, Dkt. Damas Ndumbaro
kwasababu klabu hiyo ilikiuka kanuni ilijiwekea yenyewe kwa mujibu wa
katiba.
Lugaziya amesema kuwa uamuzi wa kumrudisha
Wambura umeangali zaidi busara kwasababu Simba ilikiuka katiba yake kwa
kumuacha mwanachama aliyesimamishwa kuendelea kufanya shughuli za klabu,
na kama akiondolewa basi katiba na kamati ya uchaguzi vyote vitakuwa
batili.
“Tangu aliposimamishwa, muomba rufani
(Wambura) hajawahi kuchukuliwa kama mtu aliyesimamishwa. Kwanini?,
kupoteza haki za uanachama ni pamoja na kupoteza haki za kulipa ada,
haki za kushiriki mikutano, haki ya vikao vya maamuzi na haki ya
kuteuliwa katika vyomvyo mbalimbali vya Simba SC”. Alisema Wakili
Lugaziya.
“Tangu kutangazwa kusimamishwa, amekuwa
akishiriki shughuli za Simba. Amekuwa akishiriki mikutano yote mikuu na
dhararu, ikumbukwe kuwa mwanachama halali tu ndiye anatakiwa kushiriki
mikutano hiyo na mwanachama ambaye amesimamishwa hatakiwi kushiriki,
lakini tangu kutangaza kusimamishwa, Wambura amekuwa akishiriki”.
Alifafanua Lugaziya.
“Kubwa zaidi, mpaka sasa Wambura ni mjumbe wa
kuteuliwa wa kamati ya utendaji ya Simba na alishiriki katika mikutano
ya katiba pamoja na kushiriki kuiteua kamati ya uchaguzi”. Wakili huo
aliongeza kuwa kama mtu batili ameshiriki kufanya maamuzi, basi maamuzi
nayo ni batili. “Wambura alishiriki katika mkutano wa katiba na kuiteua
kamati ya uchaguzi, maana yake kama Wambura ni batili, basi katiba na
kamati ni batili”. Kama tunafikia maamuzi ya kusema katiba na kamati ya
uchaguzi ya Simba si halali, kwasababu mtu batili alishiriki, athari
yake ni kubwa. Kamati alishasema huko nyuma kwamba Simba ilikuwa
inamchukulia Wambura kama mwanachama”. Alisema Lugaziya.
0 comments:
Post a Comment