Mwigizaji/Mshindi wa tuzo ya Oscar Philip Seymour Hoffman amekutwa amefariki ndani ya nyumba yake usiku wa kuamkia 3/February 2014 huko mjini New York huku ikisemekana kuwa sababu ya kifo ni matumizi ya dawa za kulevya.
Vyanzo vya habari vinasema Hoffman amekutwa bafuni akiwa amevalia bukta na sindano ikiwa bado mkononi mwake.
Polisi wamekuta bahasha 10 za glassine , 2 zilikuwa dawa aina ya heroin na zingine tupu.
Askari wanasema Hoffman alitakiwa kuwapitia watoto wake jumapili asubuhi mida ya saa tatu asubuhi. Ilivyofika muda na Baba yao hakutokea ndipo ndugu wakajua kuna tatizo ukizingatia sio kawaida yake.
The following two tabs change content below.
0 comments:
Post a Comment