Jaji James Bradlin ametoa amri ya kumrudisha rehab Chris Brown kwa muda
wa siku 90 ili aendelee na matibabu ya kudhibiti hasira ikiwa ni siku
chache baada ya kutoka huko na kuendelea kuhudhuria matibabu kama
mgonjwa wa nje.
Amri hiyo imetolewa mahakamani Jumatano (November 20) kufuatia ripoti
iliyotolewa na afisa aliyekuwa anaangalia muenendo wa kipindi cha
probation alichopewa Chris Brown tangu ampige vibaya Rihanna mwaka 2009.
Ripoti hiyo ilionesha kuwa Chris alijikuta katika mood ya hasira nyingi
na kuvunja kioo cha gari la mama yake akiwa katika eneo la rehab
mwanzoni mwa mwezi huu. Lakini pia imeonekana kuwa kuna mengi yalitokea
wakati wa tukio la Breezy kumshambulia mtu October 26 huko Washington
DC.
Jaji James Bradlin pia alitoa amri inayomtaka ‘Don’t Work Me Up’ hit
maker huyo kufanya kazi za kijamii kwa masaa yasiyopungua 25 kwa wiki.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 25, akiwa na mwanasheria wake walikubali uamuzi huo bila pingamizi lolote.
Hii inamaanisha kuwa albam yake ya ‘X’ iliyokuwa inatarajiwa kutoka
mwaka huu inaweza kuchelewa zaidi kuliko ilivyotegemewa mwanzoni
kutokana na muda atakaoutumia rehab.
0 comments:
Post a Comment