Ebwana hii ndio mbinu inayotumiwa na Matajiri wa Urusi kukwepa foleni town


1Sote tunafahamu kwamba Ambulance ni magari yanayotumika kubeba na kuwaisha wagonjwa kutoka sehemu fulani kwenda sehemu nyingine na uwapo barabarani kama dereva ni lazima upishe Ambulance inayopita ili iokoe maisha ya mgonjwa ila matumizi ya Ambulance huko Urusi sio ya Wagonjwa peke yake.
Unaambiwa moja ya tabia za matajiri wa Urusi ni kukodi magari feki ya wagonjwa (Ambulance) ili kukwepa foleni hasa kwenye jiji la Moscow ambalo lipo kwenye list ya majiji yenye foleni kubwa  sana duniani ambapo matajiri hao hulipia safari moja kwa zaidi ya shilingi laki tatu za kibongo.

Ambulance hizi feki zinatofautiana na zile za hospitali kwa ndani lakini kwa nje ni kama Ambulance ya kweli ambapo hizi feki ndani yake kunapatikana huduma kama za TV, vinywaji vya aina mbalimbali, hata makochi yametengenezwa vizuri sana ambapo uzuri huo unafananishwa na magari ya kifahari ya Limousine na wakati mwingine kwenye hizi ambulance kunakua na Wanawake maalum ndani yake kwa ajili ya kutoa kampan kwa mteja.
Rais Putin na Waziri wake mkuu huwa wanapita na msafara huku magari yao yakiwa yana taa maalum za blue ambazo ni ishara kwa kila mmoja kwamba msafara wa kiongozi mkuu uko barabarani.
Polisi wamekua wakijaribu kuzisimamisha lakini sio zoezi ambalo lina mafanikio.
6
7
8
2
3
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment