NGUZO SITA ZA UMEME ZAANGUKIA BARABARA YA ALI HASSAN MWINYI JIRANI NA BAMAGA, MOTO MKUBWA WALIPUKA USIKU

Bamaga Mwenge.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Usiku wa kuamkia leo nguzo za umeme zaidi ya tano zimeanguka baada ya nguzo moja kugongwa na gari na kisha kuziangusha zingine na kusababisha moto na kishindo kikubwa kilichowashitua wakazi wa maeneo ya Bamaga Mwenge.

Tukio hilo lingeweza kuleta madhara makubwa iwapo lingetokea wakati kuna foleni ya magari kama inavyokuwa nyakati za asubuhi na jioni katika barabara hiyo ya Ali Hassan Mwinyi, jirani na maeneo ya Chuo Cha Posta, TBC1 na TSN Super Market na kituo chake cha mafuta.

Hivi sasa barabara ya Shekilango kutokea Ali Hassan Mwinyi haipitiki. Magari yaliyosababisha kadhia hii, gari ndogo na Lori la mchanga, yalikamatwa usiku lakini madereva wake walitoroka. Picha zote ni za tukio hilo kama zinavyonekana.

SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment