Rick Ross Anategemea Mauzo Bora Baada Ya Kupata Shavu Lingine Na Jay Z.


Rapper Rick Ross ametoa maelezo kuhusu wimbo utakao changia mauzo ya album yake kuwa ni wimbo na rapper Jay z unaotoka mwezi ujao.

Rozay amesema December 17 album yake ya sita 'Mastermind' inatoka na baada ya cd kuingia mtaani atatoa wimbo uliopewa shavu kubwa na rapper Jay z . Fahamu kuwa Rozay ambaye ni mwanzilishi wa record lebel ya Maybach Music Group anategemea wimbo huo kubeba na kutangaza zaidi cd yake.

Hii sio mara ya kwanza Rozay anasikika kwenye wimbo moja na Jay z, Kwenye cd mpya ya Jay z 'Magna Carta Holy Grail'  Rick Ross ameshirikishwa kwenye wimbo moja unaoitwa  "FuckWithMeYouKnowIGotIt."  na kwenye cd ya Rick Ross  'God Forgives, I Don’t' Jay z alisikika kwenye '3 Kings' iliyomshirikisha producer  Dr Dre. Rozay hajasema wimbo na Jay z unaitwaje mpaka sasa
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment