ULIOKUWA MPANGO WA KUMUUA JUSTIN BIEBER WAJULIKANA!


Naamini kwamba jina la Justin Bieber walijua na unalisikia.Kama una watoto wadogo au vijana wa rika la kati basi ndio kabisaa…Justin Bieber ndio Justin Bieber…teenagers sensation ambaye wengi wanamfananisha na Michael Jackson alipokuwa mdogo kwa jinsi alivyokuwa akikonga nyoyo za mashabiki nk.
Kwa bahati mbaya,sio kila mtu anapenda mafanikio ya huyu dogo mzaliwa wa Brantford,Ontario nchini Canada kwani ripoti zinapasha kwamba kulikuwa na mpango wa kumuua uliokuwa unasukwa na jamaa ambaye anatumikia kifungo cha maisha jela!
Wapelelezi wanasema kwamba muuaji Dana Martin ambaye inasemekana “analala na kuamka akimuwaza Justin Bieber”, alimpa kibarua au mpango mzima wa kumuua Bieber jamaa anayeitwa Mark Staake ambaye waliwahi kuwa naye jela na mpwa wa huyo Mark anayeitwa Tanner Ruane kummaliza Justin Bieber pamoja na bodyguards wake mwezi uliopita.
Dana Martin ambaye yupo jela huko New Mexico kutokana na kosa la kumbaka na kumuua msichana mdogo mwaka 2000,inasemekana aliwaelekeza Staake na Ruane kufanya mauaji hayo ya Justin Bieber jijini New York kwa kumnyonga kwa kutumia kamba. Justin Bieber alikuwa na show New York wiki chache zilizopita.
Kinachoshangaza au kustaajabisha ni kwamba Dana Martin ambaye anamuwaza Bieber kila kukicha na ambaye amejichora mguuni tattoo ya Bieber,ndiye mwenyewe aliyesababisha mpango mzima ukashindikana na kuwakamatisha jamaa ambayo alikuwa amewatuma katika sababu ambazo bado hazijawekwa wazi au kueleweka vizuri.
Mpango mzima ulikuja kujulikana baada ya Staake kukamatwa na polisi huko Vermont kutokana na makosa mengine wakati mwenzake, Ruane amekamatwa jijini New York akiwa na vifaa vya kutekelezea mauaji. Katika maongezi ya simu ambayo yamerekodiwa na polisi, Ruane ameelezea kusikitishwa na kushindikana kwa mpango huo.

SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment