La Paz, Bolivia. Mbio za kufuzu kushiriki Kombe la Dunia nchini Brazil mwakani zimepamba moto katika mabara yote duniani.
Ukanda wa Amerika Kusini (Comebol), umekuwa kazini
kwa mechi mbalimbali zilizochezwa karibuni, lakini iliyovuta zaidi
hisia za wengi ilikuwa ni baina ya Argentina na Bolivia.
Kivutio kikubwa kilikuwa ni kwa Lionel Messi ambaye alishindwa kuona nyavu, aliugua ghafla, kuishiwa hewa na hatimaye kutapika uwanjani.
Kivutio kikubwa kilikuwa ni kwa Lionel Messi ambaye alishindwa kuona nyavu, aliugua ghafla, kuishiwa hewa na hatimaye kutapika uwanjani.
Ni nini kilichomponza? Ni hali ya hewa katika
mchezo huo ambao ulichezwa mjini La Paz, urefu wa mita 4000 kutoka usawa
wa bahari. Huku, Messi mshambuliaji ambaye amefunga mabao 51 kwa klabu
yake, Barcelona msimu huu, idadi ambayo ni pungufu ya mabao mawili kwa
yale yaliyofungwa na gwiji Diego Maradona kwa nchi yake, Argentina
aliishiwa nguvu.
Maradona ambaye siku hiyo alikuwa jukwaani mjini La Paz, alimshuhudia Messi akiweweseka.
Mwenzake, winga Angel Di Maria naye pia alilazimika kupewa hewa safi ya oksijeni uwanjani katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.
Mwenzake, winga Angel Di Maria naye pia alilazimika kupewa hewa safi ya oksijeni uwanjani katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.
Kwa kawaida, Bolivia hucheza mechi za nyumbani kwenye hewa hiyo dhaifu jijini La Paz, karibu mita 4,000 kutoka usawa wa bahari.
Hali hiyo huwaathiri wapinzani wao. Wataalamu
wanaieleza hali hiyo kuwa huwapata wale wanaosafir urefu wa mita 2500 au
zaidi kutoka usawa wa bahari.
Wanaongeza wataalamu hao kuwa hali hiyo inaweza
kusababisha kuumwa kichwa, kukosa hamu ya kula na kichefuchefu (kuugua).
Pia, kutapika, kujisikia uchovu mwingi, kizunguzungu au kichwa kuwa
chepesi na kukosa usingizi.
Kwa watu wengi, dalili hizi zinaweza kupungua au kuondoka kwa kupumzika na kuizoea hali ile.
Kwa watu wengi, dalili hizi zinaweza kupungua au kuondoka kwa kupumzika na kuizoea hali ile.
Kuhusu tukio hilo la Bolivia na hali mbaya ya
hewa, Messi alisema: “Ni hatari kucheza kule, kwa hiyo sare kwetu ni
matokeo mazuri. Kila mara nilipojaribu kutembea na mpira kwa kasi,
niliishiwa nguvu, sikuwa mwenyewe.
“Baadhi ya wenzangu walisikia maumivu ya kichwa, wengine walisikia uchovu, lakini mwanzo nilikuwa vizuri.”
Bao la Bolivia lilifungwa na Marcelo Martins wakati bao la Argentina lilifungwa na Ever Banega.
0 comments:
Post a Comment