HILI NDIO JENGO AMBALO LIMEANGUKA KATIKATI YA JIJI LA DAR LEO HII





Imetokea leo hii dakika chache zilizopita Morogoro Road na Indira Gandhi (City Centre - Dar), Inasemekana Watu wapatao 60 walikuwepo ndani yake.. watoto wa Madrassa walikuwemo katika jengo hili na pia mpaka sasa maiti zilizoopolewa ni 14 na majeruhi zaidi ya 30 wamekimbizwa hospitali, Bado pia kuna baadhi ya watu hai ndani yake.

Jitihada za uokoaji zimeanza kufanyika, Waziri Nchimbi tayari amekwishafika eneo la tukio mpaka sasa japo kuna uhaba wa vyombo vinavyostahili kushughulikia hali hii.
Inasemekana majeruhi zaidi ya 30 wakimbizwa hospitalini na Maiti 14 zapatikana!! Mwenyezi mungu
azilaze roho za marehem mahali pema peponi, Amin.... Natoa pole zangu kwa wafiwa mpate nguvu katika kipindi hiki kigumu, na majeruhi nawatakia kupona haraka!!
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment