Dar es Salaam: Askofu Mkuu wa
Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam Kardinali Polycarp Pengo jana
aliongoza ibada ya Alhamisi Kuu huku kukiwa na ulinzi mkali
uliowajumuisha polisi waliovalia sare na wale kawaida, ikiwa ni siku
moja baada askofu huyo kulituhumu jeshi hilo kwa kutowajibika ipasavyo.
Askari hao walikuwa wamegawanyika katika makundi
mawili ambao baadhi yao walionekana wakirandaranda eneo la nje ya Jengo
la Kanisa la Mt. Joseph ambako ibada hiyo ilifanyika huku wengi walikuwa
ndani ya kanisa walikojumuika na waumini wa kawaida.
Haikuweza kufahamika mara moja sababu za
kuimarishwa kwa hali ya ulinzi, lakini baadhi ya vyanzo vya habari
vilieleza kuwa, hali hiyo imejitokeza kama sehemu ya kujaribu
kukabiliana na hali yoyote hasa kutokana na vipeperushi vilivyosambazwa
siku za chache zilizopita.
Pengo alikuwa akiendesha ibada ya Alhamisi Kuu ambayo Yesu Kristu alikuwa akifanya ibada hiyo kwa kuwaosha miguu mitume wake.
Ibada hiyo ilifanyika dunia nzima kwani hata Papa
Francis alifanya kazi hiyo kwenye Makao Makuu ya Kanisa Katoliki kwenye
Mji wa Vatican, Italia.
Siku chache kabla ya kuingia msimu wa Sikukuu ya Pasaka inayoanza leo kwa Ijumaa Kuu,
vilisambazwa vipeperushi vilivyokuwa na ujumbe wa kuvuruga ibada za Pasaka , hatua ambayo ilisababisha Jeshi la Polisi kutoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la uvunjifu wa amani.
Ibada ya Sikukuu ya Pasaka kitaifa imepangwa kufanyika mkoani Dodoma.
vilisambazwa vipeperushi vilivyokuwa na ujumbe wa kuvuruga ibada za Pasaka , hatua ambayo ilisababisha Jeshi la Polisi kutoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la uvunjifu wa amani.
Ibada ya Sikukuu ya Pasaka kitaifa imepangwa kufanyika mkoani Dodoma.
0 comments:
Post a Comment