Dar es Salaam. Kamati
iliyoundwa na Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai kuchunguza tuhuma za
kuwapo kwa danguro na uuzaji wa dawa za kulevya katika eneo la Kipawa
jana ilijikuta inashindwa kutimiza malengo yake baada ya baadhi ya
wakazi wa eneo hilo kuwatimua wajumbe huku wakiwatishia kuwadhuru kwa
zana mbalimbali yakiwamo mapanga.
Hatua hiyo imekuja baada ya kamati hiyo kugundua
kuwa baadhi ya wanafunzi wanatoroka shuleni na kwenda kununua dawa hizo
ikiwamo bangi na eneo ambalo wanafunzi wanakwenda kufanya ngono.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti
wa Wazazi katika shule hiyo, Said Magubige, alisema walikubaliana kwenda
katika eneo hilo ili kuwabaini wale wanaotumia nyumba zao kuwapokea
wanafunzi wanaojihusisha na vitendo vya ngono na biashara ya dawa za
kulevya.
“Kamati yetu ilipokwenda kufuatilia, tulishangaa
kuona umati wa watu wanaokaa kwenye nyumba zilizopo karibu na shule hii,
wakitufukuza kwa mapanga huku wakitoa maneno ya kutishia
maisha,”alisema Magubige.
Alisema baada ya kutokea hayo walitoa taarifa
kwenye Kituo kidogo cha Polisi cha Stakishari lakini hakuna hatua
iliyochukuliwa na matokeo yake watoto wanazidi kuharibika.
Mkuu wa Sekondari hiyo, Jansinta Assey, alikiri na
kusema kwamba vitendo vya uvutaji wa bangi na biashara ya ukahaba kwa
wanafunzi wake vinachangiwa na askari wa Kituo kidogo cha Polisi cha
Stakishari ambao alidai wanachukua rushwa kwa wauzaji hao na nyumba bubu
za wageni.
Assey alisema ni kawaida ya polisi hao kwenda
kwenye nyumba kunakofanyika biashara hizo na kuchukua rushwa badala ya
kutatua tatizo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema hajapata taarifa za hali hiyo.
”Ngoja nimtume mkuu wa polisi wa kituo hicho ili afuatilie”alisema Minangi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema hajapata taarifa za hali hiyo.
”Ngoja nimtume mkuu wa polisi wa kituo hicho ili afuatilie”alisema Minangi.
0 comments:
Post a Comment