VIKOSI VYA MAJESHI VINAVYOONGOZWA NA UFARANSA KASKAZINI MALI VIMEDHIBITI MJI WA TIMBUKTU

Vikosi vya majeshi vinavyoongozwa na Ufaransa kaskazini mwa Mali vimeudhibiti mji wa Timbuktu katika harakati za kukomboa eneo la kaskazini mwa Mali kutoka mikono ya wanamgambo wa kiislamu wanaohusishwa na kundi la kigaidi la Alqaeda.
Makamanda wa jeshi la Ufaransa wanasema kuwa wanajeshi wanafanya doria kwenye barabara za miji wakilenga kuwafurusha wapiganaji waliosalia.
Pindi mji wa Timbuktu utakapokombolewa, wanajeshi wanatarajiwa kulenga kuwaondoa waasi katika eneo ambalo linakaliwa na waasi la na ngome yao Kidal.
Wakati huo huo mkutano wa wafadhili wa Mali unatarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Ethiopia -Adis Ababa hii leo kuchangisha pesa kwa ajili vikosi vya kimataifa vinavyopigana dhidi ya waasi wa Kiislam.
Gharama za kuendesha harakati za kijeshi nchini Mali zinakadiriwa kuwa kati ya dolla milioni mia tano na dola bilioni moja .
Huku ahadi za misaada zilizotolewa hadi sasa na Mataifa ya Afrika na muungano wa ulaya zikiwa ni dola milioni moja, zaidi ya wahisani sitini walioalikwa katika mkutano huo wanatarajiwa kuziba pengo hilo.
Na Mkutano mwingine unafanyika mjini Brassels kuamua juu ya kutumwa kwa kikosi cha muungano wa ulaya cha kutoa mafunzo kwa askari wa serikali ya Mali.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment