Leo hii Steve rnb amefunguka juu ya utata uliokuwepo kati ya producuer
wa Combination sound, Man Walter, na kampuni ya KVelli, ambapo kila
mmoja kwa wakati tofauti amedai kusimamia kazi zake.
steve rnb ambae kwa sasa yuko nchini Uholanzi, amefunguka na kusema,
"Man Wolter na hisi yeye alikua hajaweka wazi, na mimi mwenyewe nilikua
bado sijamuelewa, kwasababu wakati mi nimetoka Ujerumani nilikubaliana
nae kusimamia ngoma ya "radio" niliyofanya na Ommy Dimpoz,ambapo mikataba yote ilikua kwenye huo wimbo,
sasa mimi nilifanya jambo jambo kwa nguvu zangu mwenyewe, kwa bahati
nzuri nikapata wadhamini ambao ni hao washkaji, vijana wenzagu KVelli,
nikaamua nifanye nao kazi, na nikasaini nao mkataba, na kila kitu kipo
kamili, tulikua tunakamilisha mambo madogo madogo kama loya na
vinginevyo lakini kila kitu kitakua tayari by tommorow. huo ndio
ukweli." amesema Steve rnb.
Licha ya hivyo vyote, K Velli wametangaza kuachia single nyingine mpya
kutoka kwa Steve rnb hivi karibuni special kwa ajili ya valentine.
0 comments:
Post a Comment