PROFESA MWANDOSYA ANENA YA MOYONI


Na Profesa Mark Mwandosya
Leo ni siku inayofuatia jana, siku ambayo Ndugu yangu Edward Ngoyai Lowassa aliacha rasmi uanachama wa CCM na kupewa kadi ya uanachama wa Chadema. Si yeye tu bali alisindikizwa na mke wake mpendwa Mama Regina Lowassa. 
Nilidhani leo mitandao yote ingesheni habari hiyo kubwa. Kumbe nami nimekuwa "staa" katika mitandao ya kijamii. Kuanzia asubuhi nimekuwa nikipokea na kujibu simu mbalimbali nikiulizwa maoni yangu kuhusu tukio la jana, kuhusu mchakato wa Dodoma uliomalizika hivi karibuni, na "habari" kubwa imekuwa Mwandosya, Mwapachu na ole Medeye wahamia Chadema! 
large;">Kuhusu Ndugu Lowassa kuhamia Chadema nionavyo mimi ni jambo la kawaida sana katika demokrasia ya vyama vingi. 
Wanachama hutoka na kuingia karibu kila siku. Hivyo basi tukio la jana lisingegonga vichwa vya habari kama isingekuwa kwa umaarufu wa mhusika. Jambo la msingi kwa CCM ni kutafakari, bila ghadhabu, na kwa utulivu, ni sababu zipi za msingi zilizofanya hili jambo litokee? Je tunaweza kujifunza lolote katika hili ili kukiimarisha Chama? 
Tunaweza kuboresha nini katika taratibu na kanuni zetu? Nimeulizwa pia kitendo cha Ndugu Lowassa kuhamia Chadema kina athari gani kwa CCM? 
Pamoja na kutotokuwa msemaji rasmi wa Chama, tukio hili lina maslahi ya umma kwa ujumla hivyo kukwepa kujibu hakusaidii. Siasa ni takwimu, hasa tunapoelekea Oktoba. Kwa mantiki hiyo mtu mmoja kukihama Chama kuna maana kura moja iliyopungua
Kwa kuwa haiwezekani kuirudisha, basi changamoto ni kuwa na mkakati wa kutafuta kura ya kufidia, kuzuia kupotea kwa kura nyingine, na kuongeza idadi ya wanaoingia ili iwe kubwa kuliko ile ya wanaotoka. 
Msaafu wa dini unasema mchungaji bora ni yule anayeweza kuwaacha kondoo wake tisini na tisa walio salama ili amtafute yule mmoja aliyepotea! Suala la kujiuliza katika mazingira ya yaliyotokea ni je tulikuwa wachungaji bora? 
Nadhani moja ya mambo ya msingi CCM itabidi tulitafakari kuhusiana na mchakato wa kumpata mgombea wetu kwa nafasi ya urais ni je tunamtafuta mwanachama ambaye atakuwa Rais? Je tunamtafuta mtu ambaye atakuwa Rais wa nchi na Mwenyekiti wa Chama? Au tunamtafuta mtu atakayekuwa Rais na Waziri Mkuu? 
Vigezo vya kumtafuta mtu huyo vinapishana kama ambavyo orodha wa wenye nia au mifumo ya kumpata itapishana. Naamini tungelitafakari haya yote huenda tusingefika hapa tulipo. Lakini Taifa ni kubwa kuliko sisi watu na uhai wake ni mpaka "kiama cha wafu". 
Tujadili masuala haya na mengine muhimu, kwa ujasiri, uwazi na ukweli. Nahitimisha kwa kujibu taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na watu wengi ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari kuhusu Mwandosya kuhama kwenda Chadema. 
Misingi iliyojengwa na waasisi wa Chama, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume naendelea kuamini bado ni sahihi. Ndiyo iliyotuletea heshima kubwa kama Taifa. 
Kama tumeyumba turudi katika misingi. Itikadi ya Chama inajengwa juu ya misingi hiyo. Hivyo basi kwangu mimi Ilihali misingi ipo, na imara, nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM ili kwa pamoja na wanachama wenzangu tuendelee kulijenga Taifa juu ya misingi hiyo, kila wakati tukikumbuka kile alichotuasa Baba wa Taifa, Tujisahihishe!
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment