Mara
nyingi stori za aina hii huanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii,
baadae unaona RADIO na TV nazo zinaanza kuripoti.. Siku ya leo APRIL 9
watu walianza kusambaziana picha za ajali iliyotokea Tanga, mabasi
mawili ya abiria na gari dogo yamegongana, watu 10 wamefariki na wengine
kujeruhiwa.. kabla siku haijaisha naipokea hii nyingine kutoka
Morogoro.
Basi la Kampuni ya Happy Nation lenye namba T 618 BDN lililokuwa likitokea Dar es Salaam
kuelekea Mbeya limepata ajali hiyo eneo la Mikumi, Morogoro.. taarifa
za awali zinasema watu wawili wamefariki na wengine kujeruhiwa.
Chanzo cha ajali hakijafahamika, naifuatilia hii kwa ukaribu.. kitakachonifikia nitakusogezea hapa muda wowote mtu wangu.
#RIP kwa watu wetu waliofariki kwenye ajali hiyo, pole kwa waliopata majeraha pia.
0 comments:
Post a Comment