Matukio hayo yanayoliweka Taifa katika wasiwasi
zaidi hasa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, yamekuwa
gumzo kila kona ya nchi kutokana na utata wake.
Tukio la Tanga
Katika mfululizo wa matukio hayo, juzi risasi
zilirindima mkoani Tanga kwa zaidi ya saa 48 wakati Polisi na askari wa
JWTZ waliposhirikiana kupambana na wahalifu hao.
Katika mapambano hayo, askari mmoja wa JWTZ alipoteza maisha na wapiganaji wengine zaidi ya sita kujeruhiwa.
Jana, askari hao waliendelea na operesheni ya
kuwasaka watuhumiwa na hadi tunakwenda mitamboni hakukuwa na taarifa
zozote za kukamatwa kwao.
Mbali na kutokamatwa watu hao ambao hawajajulikana
ni wahalifu wa aina gani, pia silaha zilizokuwa zinasakwa hazikukutwa
kwenye Mapango ya Amboni kama ilivyokuwa ikihisiwa, zaidi ya pikipiki
moja mbovu na baiskeli tatu. Habari zilizopatikana jana zimedokeza kuwa
vikosi vilivyopo katika operesheni hiyo vimebadili mbinu za kuwasaka
majambazi hao.
Vilevile, wakazi wa kitongoji cha Karasha Amboni
ambao walihama kukimbia mapigano, hadi jana walikuwa hawajarejea
majumbani mwao.
Majeruhi
Kwa upande wa majeruhi waliolazwa katika Hospitali
ya Rufaa ya Bombo, wanaendelea na matibabu huku madaktari na wauguzi
wakitakiwa kutoa taarifa za kila anayefikishwa hapo akiwa majeruhi.
“Tumepewa maelekezo kwamba kila raia anayefikishwa
hapa akiwa na majeraha tutoe taarifa haraka kwa uongozi kwani kuna
uwezekano wa kuletwa waliofanya mashambulizi kwenye mapango,” alisema
mmoja wa wauguzi kwa sharti la kutotajwa jina.
Wakazi wa Kijiji cha Kiomoni kilicho jirani na
mapango ya Amboni, walisema baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa
vikipotosha taarifa juu ya eneo yalikofanyika mapambano, kwamba ni
mapango ambayo hutembelewa na watalii na wageni wengine, wakati si
kweli.
0 comments:
Post a Comment