Tottenham Hotspurs wamefanikiwa kuwafunga Arsenal katika mchezo wa ligi kuu ya England uliopigwa hii leo (Jumamosi) kwenye uwanja wa White Hart Lane ukiwa mchezo wa kwanza wa ligi hiyo kwa ratiba ya jumamosi .
Arsenal ndio walianza mchezo huo kwa kasi zaidi wakipata bao la kwanza kupitia kwa kiungo mshambuliaji Mesut Ozil ambaye alifunga kwenye dakika ya 11 .
Spurs walisawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji chipukizi Harry Kane ambaye alifunga kwenye dakika ya 56 ya mchezo zikiwa zimepita dakika 9 tangu kuanza kwanza kipindi cha pili .
Kane aliwahakikishia Tottenham pointi zote tatu kwenye dakika ya 86 kwa kufunga bao la pili bao ambalo limewapaisha Spurs mpaka kwenye nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.
Kane hadi sasa amefunga mabao 12 kwenye ligi hiyo ambapo anashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa wafungaji akiwa nyuma ya Diego Costa , Sergio Aguerro na Charlie Austin .
0 comments:
Post a Comment