Zoezi la kuandikisha upya wapiga kura wenye sifa, kwa kutumia mfumo
mpya wa kidigitali au kielektroniki, yaani Biometric Voters Registre,
(BVR), limeanza jijini Dar es Salaam kwa majaribio, na hakika hakuna
longolongo wala kupoteza muda, Mimi nimeshuhudia mtu mmoja humchukua
takrivan dakika 10 tu kupatiwa kitambulisho au kadi ya kisasa ya kupigia
kura. Hatua hizo ni kama zifuatazo, mosi, mtu anayeomba kuandikishwa
ataonyesha kitambulisho na kujaza fomu ya Tume ya Uchaguzi ya kuomba
kuaandikishwa, baada ya kujaza fomu hiyo hatua ya pili ni kuipeleka kwa
muandikishaji msaidizi namba 2 ambaye ataingiza kumbukumbu hizo
zilizomokatika fomu kwenye computer, hatua itakayofuata ambayo ni ya
tatu, mtu huyo atatakiwa kuweka dole gumba na vidole vyake vitano ili
viweze kuchukuliwa alama zake yaani scanned, baada ya hapo hatua
inayofuata ni muombaji kupigwa picha na mwisho kabisa ni kupatiwa kikadi
yaani kadi ya kupigia kura, kwa hakika inafanana sana na kitambulisho
cha taifa, kama umekwishakipata. Zoezi hilo kwa mujibu wa tume ya taifa
ya uchaguzi NEC, litaanza rasmi nchi nzima kuanzia Februari mwaka 2015
ambao ndio mwaka wa uchaguzi mkuu
Mwandishi msaidizi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa, (NEC), ambaye kwa
sasa watajulikana kama BVR Operators, akijaza fomu ya mtu anayeomba
kuandikiswa kupiga kura leo Jumanne Desemba 16, 2014, plae Bunju A,
wilaya ya Kinondoni jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam
Muombaji (Kulia), akijaziwa fomu kabla ya kuendelea na hatua zingine
Muombaji (Kulia), akikabidhi fomu aliyojaziwa katika hatua ya kwanza ya kuomba kuandikiswa
0 comments:
Post a Comment