Dapo Daniel Oyebanjo a.k.a D’Banj amekuwa Balozi wa bidhaa za Beats by Dre
kwa upande wa Afrika kwa miezi kadhaa sasa, dili linalomfanya aongeze
ile mirija ya kujaza akaunti zake za Benki Naira nyingi tu kila mwezi.
Beats by Dre zina heshima yake kubwa sokoni kwa sasa, najua unajua hilo, kingine ni kwamba kuna zile special
ambazo huwa zinatengenezwa chache na maalum kabisa, mtu ambaye anaweza
kupewa labda ni Balozi wao au mtu mwingine maalum kama zawadi, kama
ikitokea zikiuzwa basi bei yake huwa ni bei maalum vilevile.
Katika zile special ambazo zimewahi kutolewa kwa Balozi D’Banj, aliwahi kumpa zawadi ya aina hiyo Iyanya wakiwa Airport Nigeria, baada ya hizo taarifa ikufikie kwamba safari hii zali hilo limemuangukia Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan.
Kaweka picha Instagram (iambangalee)
akimvalisha Mr. President mzigo huo, mitandao ya Naija haikukosa neno,
wanasema eti Rais alionekana kama hakuipokea poa hii ya kuvalishwa
headphone hizo, huenda Balozi huyo alikiuka protocol labda.
Aliandika hivi kwenye post hiyo; “Merry Christmas Mr President with Love from@iambangalee and @Beatsbydre OooSssHhhEee“– @iambangalee
Cheki tukio zima hapa.
0 comments:
Post a Comment