Kutoka Dodoma 104.4 kabla ya kujadiliwa kwa bajeti ya wizara ya afya
na ustawi wa jamii ilianza sehemu ya maswali na majibu kuanzia saa tatu
asubuhi mpaka saa nne.
Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Juma Nkamia ndio alijibu
swali la Catherine Magige kuhusiana na udhalilishaji wa Wanawake
unaofanywa kwenye kumbi mbalimbali za starehe Tanzania.
Waziri
Nkamia alisema ‘nakubalia kabisa kwamba kumbi za starehe zimekua
zikitoa burudani na ajira kwa vijana hapa nchini lakini ndani ya kumbi
hizo kumekua na vitendo vinavyofanyika kinyume na maadili ikiwemo
udhalilishaji wa Wanawake’
‘Katika kukomesha hali hiyo serikali kupitia baraza la sanaa BASATA
wamefanya vikao kadhaa na wamiliki wa bendi, maafisa utamaduni, wakuu wa
polisi, wamiliki wa kumbi na wanaojihusisha na uchezeshaji wa mtindo wa
kanga moja ili kujadili ukiukwaji wa maadili kwenye sanaa’
Kwenye sentensi ya tatu Waziri anasema ‘Pia serikali imeacha kutoa
usajili kwa vikundi kama cha kanga moko kwa kuwa uchezaji wake unakwenda
kinyume na maadili ya Tanzania na kutoa onyo kwa wamiliki wa kumbi,
Wasanii na hata asasi zinazojihusisha na sanaa ambazo hazifati maadili’
Anasema ‘Wasanii waliopewa Onyo ni Ney wa Mitego, Shilole, Wema
Sepetu, Aunt Ezekiel na kwa upande wa kumbi ni Mama’s and Papa’s lakini
pia maonyesho ya urembo ya Miss Utalii yalifungiwa ambapo pia Serikali
imeunda kamati ya kitaifa ya kuzuia ukatili na unyanyasaji dhidi ya
Wanawake/Wasichana watoto’
Home
Aunt Ezekiel
Shilole na Ney wa mitego walipotajwa bungeni.
wema sepetu
Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Shilole na Ney wa mitego walipotajwa bungeni.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment