Macho
na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote
yalielekezwa Durban Afrika Kusini sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo
za wateule wa MTV Afrika Music Award ‘MAMA’.
Furaha tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana
kutoka nyumbani Tanzania kuwa ni miongoni mwa vijana wanaochuana kwenye
tuzo hizo tena akiwa vipengele viwili,ingawa bahati haikua njema kwa
Diamond kwani hakufanikiwa kupata.
Baada
ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimaond Platnumz
ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya
kijamii>’Maisha ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa
hatua yetu kwa MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi
tulipo leo… pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next
tym tuzidi kufanya vyema…. Shukrani zangu nyingi ziende kwa Mashabiki
wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa
nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda
nyingine…Next stop #BET!!!… Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii’.
Diamond Platnumz alikuwa pia ni moja kati ya watumbuizaji wa ugawaji
wa tuzo hizi,ambapo kwa namna alivyoingia kwenye jukwaa na Davido
ilimfurahisha kila mtu aliyekuepo ukumbini na watu waliokuwa wakiangalia
nyumbani kupitia DSTV
Home
Neno la kwanza la Diamond Platnumz baada ya kutofanikiwa kuchukua tuzo za MTV MAMA.
Neno la kwanza la Diamond Platnumz baada ya kutofanikiwa kuchukua tuzo za MTV MAMA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment