Kama ulikuwa hufahamu basi skia nikwambie, collable ya Diamond na Davido
"Number one Remix" ndio imeanzisha safari kubwa yakutambulika kwa
Diamond Africa na nje ya Africa mpaka kumpelekea kuchaguliwa katika tuzo
za MTV MAMA na BET
Sasa kali kuliko hiyo ni pale ambapo inaonekana kunukia kwa safari ya
kimataifa zaidi kwa mtu mzima Diamond na hasa kunukia kwa collable ya
kimataifa zaidi.
Sasa
kolabo inayonukia sasa hivi ni ya staa wa muziki kutoka Marekani ambae
ni Trey Songz ambae taarifa za ndani zinadai kwamba kama kolabo hii
ikifanikiwa basi Rais Kikwete atakua ameshiriki kuiunganisha kwa
asilimia zaidi ya 90.
Kwenye picha
President ameonekana akiwa karibu sana na meneja wa Trey Songz na
waliongea kwa kirefu, kwa sababu President siku zote anasupport sana
Wasanii wake wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment