Joh Makini aeleza alichojifunza kwenye show ya P- Square, je anadhani ni show bora zaidi kuwahi kufanyika Dar? Anajibu hapa


13Mwamba wa Kaskazini Joh Makini ambaye aliungana na wasanii wa kundi la Weusi Jumamosi (November 23) na kudondosha show kali na kulipamba tamasha la ‘P-Square Live In Dar’, ameeleza vitu alivyojifunza kwenye performance ya wasanii hao ndugu toka Naija, Peter na Paul.
Joh ameiambia tovuti ya Times fm kuwa amejifunza zaidi jinsi ya kuwasiliana na audience wake wakati anaimba jukwaani na kuwafanya wawe wajisikie kuwa sehemu ya show.
“Kitu ambacho nimejifunza ni kwamba kuendelea kuongeza confidence na jinsi ya ku-communicate na fans unapokuwa jukwaani ndio kitu kikubwa zaidi kwenye show mbali na muziki unaokuwa unaufanya pale. Kuongea na watu na kuwacheck wako kwenye mood gani na kurelax kwenye stage ndio kitu ambacho nimejifunza. Kwa sababu hata ukiangalia show ya P-Square utagundua wao wana confidence wanapokuwa kwenye jukwaa wanaongea na watu. Inawafanya fans wanajisikia wako na wewe kwenye lile tukio sio tu unapiga wimbo baada ya wimbo unaondoka.”
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment