Frank Mtao awa mwenyekiti wa watanzania nchini Australia



Mmiliki wa kampuni ya 2 Eyez Production na aliyewahi kuwa mtangazaji wa kituo cha television cha channel ten Bw. Frank Mtao, Jumamosi iliyopita Novemba 23 alifanikiwa kunyakua kiti cha uenyekiti wa chama cha Jumuiya ya Watanzania waishio New South Wales nchini Australia.

Katika kinyang'anyiro hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Lethington uliopo kitongoji cha Summer Hill, mjini Sydney, Frank alifanikiwa kumshinda mpinzani wake ambaye ni mkazi wa muda mrefu katika jiji la Sydney Bw Christopher Banda kwa kura 55 dhidi ya 6 alizozipata Chriss.

Baada ya ushindi huo mzito,Frank aliwashukuru wanachama wote kwa kujitokeza kwa wingi na kufanikisha sherehe hizo za kufunga mwaka na uchaguzi na pia aliwapongeza wengine waliochagulia katika bodi yake ya chama hicho na kuhaidi watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuwahaidi kuongeza jitihada za kuwakutanisha Watanzania hao na kusaidiana kwa kila hali!

Kwa upande wa msaidizi wa Frank yaani nafasi ya ukatibu ilikwenda kwa Louis ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara mkubwa Tanzania Bw. S.H Amoni.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment