Kwa mara ya pili mfululizo, wasanii wa Nigeria wanaowania Tuzo za MTV
katika category ya Africa wameondolewa katika mashindano hayo.
Waandaaji wa Tuzo hizo wametangaza kuwa wasanii wa South Africa, LCNVL
wamepigiwa kura kama Best African Act, position iliyowaondoa WizKid na
P-Square katika mashndano hayo. Mwaka jana Wizkid na D'banj walikuwa ni
washiriki pia kutoka Nigeria ambao hawakupita pia.
Kwa wiki sita zilizopita MTV waliwapa mashabiki nafasi ya kupiga kura
kwa wasanii wao wa nyumbani wanaowapenda kuwasaidia kupata "The Best
Act" tittle kupitia wao. LCNVL sasa wamesogea katika hatua ya pili ya
kupigiwa kura ili kujaribu kupata nafasi ya kuwakilisha wanapotoka
katika World Wide Act category katika Tuzo hizo zitakazo fanyika siku ya
jumapili, ya November 10, Amsterdam.
LCNVL inayoundwa na mapacha wawili, Brian na Andrew Chaplin wamekuwa ni
wasanii maarufu na wenye mafanikio makubwa nchini SA kwa miaka 5 sasa,
wakiwa wameuza zaidi ya copy 100,000 ya album zao, wameshinda Tuzo za
SAMA (South African Music Awards) kama album iliyouza sana tuzo ya
wasanii wapya (Best Newcomer) na kufanya tua duniani wakiwa na Justin
Bieber, Tiao Cruz, Mike Poser na Jason Darulo.
kuanzia sasa LCNVL watachuana na Honey Singh (India) na Ahmed Soultan
(MIddle East) katika nafasi ya 10 bora watakaoingia katika category ya
Worldwide Act.
Ripoti zinadai kuwa Miley Cyrus, Robin Thicke, Snoop Dogg, Afrojack,
Imagine Dragons, The Killers na Katy Perry wanategemewa ku-perform
katika MTV EMA 2013.
Hivi karibuni Wizkid ameachia video ya wimbo wake "Jaiye jaiye" itizame hapo chini
0 comments:
Post a Comment