Rapper maarufu South Africa na mshindi wa tuzo kadhaa, amekoswa koswa
kuuwawa baada ya kurushiwa risasi kadhaa na polisi Johannesburg asubuhi
ya leo wakidhani ni mshukiwa wa utekaji nyara.
Khuli Chana ambae jina lake halisi ni Khulane Morule, alikuwa amesimama
katika kituo cha mafuta akitaka kujaza mafuta kwa ajili ya kuelekea
Pretoria kwa ajili ya kufanya show, kwa bahati mbaya ikatokea kuwa kituo
alichokuwepo ndio hicho kilichochaguliwa kama ni sehem ya kitovu cha
uhalifu huo.
Polisi waliokuwepo katika eneo hilo waliarifiwa kuangalia gari ya kijivu
aina ya BMW kama gari la mtekaji nyara huyo.Chana alikuwa akiendesha
BMW yenye rangi ya blue wakati huo, na baada ya kutokusimama katika eneo
la polisi ambalo halikuwa rasmi, gari la Rapper huyo, lilirushiwa
risasi 6 za onyo, Chana alipatwa na risasi katika kidole na mgongoni,
ambapo saa hii anaugulia nyumbani kwake baada ya kuruhusiwa hospitali.
"Ukweli wa mambo huu ni ukatili wa polisi," amesema Manager wa Chana
Refiloe Ramogase. " Polisi wanahitaji kuwa na tahadhari zaidi kabla ya
kutumia nguvu ya kuuwa."
Tukio hilo kwasasa linachunguzwa na Independet Police Investigative Directorate.
Chana aliondoka na tuzo 3 za tuzo za mziki wa South Africa mwezi wa 5
ikiwemo albam bora ya mwaka "Lost in Time" ikiwa ni maraya kwanza kwa
msanii wa Hiphop kuchukua tuzo hiyo katika historia ya tuzo hizo
zilizoanzishwa miaka 19 iliyopita.
0 comments:
Post a Comment