WAGANGA
wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja wamenaswa jijini Mwanza
wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoamainika kuwa wa binaadamu
ambapo walikamatwa kwenye eneo la ziwani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na kufanikiwa kuwakamata.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Joseph
Konyo amethibitisha tukio hilo na kwamba mkono huo uliokuwa umewekwa
kwenye begi ukiwa umefungwa kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na
kuviringishwa kwenye karatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
kwa mujibu wa makubaliano hayo wauzaji hao ambao ni Waganga walitaka
kupewa shilingi milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya
mazungumzo ya kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei
na kujikuta wakitiwa mbaroni baada ya kuonyesha kiungo hicho.
Konyo
ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO),
alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka
36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
Taarifa
zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya
kununua viungo hivyo kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji),
walimhakikishia mnunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata kichwa, mikono,
miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo mteja angehitaji.
0 comments:
Post a Comment