Eminem Yuko Tayari Kutoa Wimbo Mwingine Mkubwa Aliomshirikisha Rihanna.Sio mara ya kwanza kusikia vichwa hivi viwili kwenye wimbo mmoja, walishawahi kusikika kwenye Love The Way You Lie, Love the Way You Lie 2 na Numb zilizotoka Mwaka Jana na kushika namba moja kwenye chati nyingi za nyimbo bora duniani.
Eminem anatarajiwa kutoa wimbo kutoka kwenye album yake mpya ya The Marshall Mathers LP 2 ambao kashirikishwa mwanadada Rihanna. Wimbo huu unaitwa  "The Monster" na inasemekana Rihanna kafanya maajabu tena. Wimbo huu unatoka tarehe 5 November.

Rihanna alizungumza na Complex mwanzo wa mwaka huu nakusema kuwa mara ya kwanza amefanya kazi na Eminem alifurahi sana na alitaka tena kufanya nae kazi. Riri amesema anapenda kusikiliza mashairi ya Eminem na anakubali uandishi wake.

SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment