Bondia Rashid ‘Snake man’ Matumla |
Mkwanda amewahi kugombea ubingwa wa dunia wa IBF kwa vijana mara mbili.
Dar es Salaam: Bondia Rashid ‘Snake man’ Matumla amedai endapo itathibitika mdogo wake, Mkwanda anajihusisha kusafirisha dawa za kulevya atakuwa ameipa fedheha familia yao.
Dar es Salaam: Bondia Rashid ‘Snake man’ Matumla amedai endapo itathibitika mdogo wake, Mkwanda anajihusisha kusafirisha dawa za kulevya atakuwa ameipa fedheha familia yao.
“Mkwanda ameipa fedhea familia yetu, hii ni aibu kubwa ukizingatia
vitendo hivyo vinakatazwa si Tanzania tu bali na kwenye nchi nyingine,”
alisema Matumla jana katika mahojiano na gazeti hili.
Mkwanda ambaye kwa mujibu wa Rashid alipumzika kucheza ngumi miaka
kadhaa iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi alikamatwa wiki
iliyopita nchini Ethiopia akiwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Joseph
Kaniki na leo watapandishwa kizimbani nchini humo kwa tuhuma hiyo.
“Mimi mwenyewe nashangaa ni lini amejiingiza kwenye kazi hiyo, hata
wakati anaondoka hakuniaga, mimi kaka yao na familia hatuelewi
chochote,” alisema Matumla.
Alisema mdogo wake huyo alikuwa amebadilisha uraia na kuchukua uraia wa
Sweden na kuoa hukohuko Sweden licha ya kwamba hapa Tanzania alikuwa
amepanga Mbagala, Dar es Salaam na alikuwa anakuja na kukaa kwa muda na
kisha kuondoka.
“Ni mwezi sasa umepita sina taarifa naye na hata wakati anaondoka
hakuniaga, nimesikia kupitia vyombo vya habari kitendo cha mdogo wangu
kukamatwa kimenisikitisha mno, siyo siri nimekwazika na ninarudia kusema
hii ni fedheha kwenye familia yetu,” alisema bingwa huyo wa zamani wa
dunia wa WBU. Rekodi zinaonyesha kabla ya kupumzika kwa muda kucheza
ngumi, Mkwanda alishinda mapambano manane (sita kwa KO) alipigwa mara
tatu zote kwa KO alitoka sare mara moja tangu 2004.
0 comments:
Post a Comment