Mashairi Ya Wimbo Mpya Wa Kala Jeremiah Ft Mary Lucos - Jaribu KujiulizaWIMBO JARIBU KUJIULIZA
MSANII KALA JEREMIAH ft MARY LUCOS
MUANDAAJI NAH REEL
MPIGA ZEZE NG'WANASHIJA
STUDIO HOME TOWN RECORDS

INTRO THANK YOU GOD IS ANOTHER DAY
IM ALIVE NO STRESS NO PAIN
YAH LET ME WORK IT OUT, NAH REEL.

UBETI WA KWANZA


WE MWANADAMU JARIBU KUJIULIZA
UNGEKUWA MUNGU NI NANI UNGEMSIKIZA?
POLISI WA DORIA AU KIBAKA NDANI YA GIZA?
JE NI NANI ANGEPOKEA MIUJIZA?
MLEVI WA GONGO AU MAMA ANAYEUZA?
YOOTE TISA UNGEMPONYA MGONJWA NDANI YA MACHELA?
PAPI KOCHA SEYA WANGEGEUKA PAUL SILA?
AU UNGELALA NA KUZUGA HUTUONI MAFUKARA?
SIMBA ANAKUOMBA WEWE KABLA YA KUMUWINDA SWALA
SWALA ANAFANYA SALA UMUEPUSHE NA MISALA
JE? UNGEKUMBUKA KUWA MBU HAJALA?
UNGEMKUMBUKA MWANAID WA MBAGALA?
TUMA ANAKUOMBA WEWE KABLA YA KULALA
WAKATI JAMBAZI SUGU YUKO NJE ANAFANYA SALA
ANAOMBA TUMA ALALE FOFOFO USIWE MSALA
JE? UNGENIPA MKE MWENYE UPENDO KAMA WASTARA AU UNGENISAKIZIA CHANGU MWENYE PENZI LA BIASHARA?
UNGEKUWA MUNGU UNGESHAMEZA SUMU
AU UNGESHATUCHOMA MOTO KUYAKWEPAA MAJUKUMU.

KIITIKIO

JARIBU KUJIULIZA,JARIBU KUJIULIZAAAA
JE? UNGEKUWA MUNGU, WOOH OUWOOH
JE? UNGEKUWA MUNGU WEEEEE
JE? UNGELISHA NDEGE WA ANGANI WEEEE
JE? UNGETUPA PUMZI BURE WEEE.OOOH OUWOOH

UBETI WA 2

uNGEIJUA KESHO NA KESHOKUTWA
UNGESHUHUDIA MKONO WA ALBINO UKIKATWA
NA MKATAJI AKIKULILIA ASIJE KUKAMATWA
UNGEKUWA MUNGU NAHISI UNGESHADATA
KUNA KINA MARIAM NA LAMATA
WANATAKA NDOA NA WACHUMBA HAWAJAPATA
MUNGU SINA KAZI NA NATAKA KULA BATA
JE KWELI UNGEMKUMBUKA YULE NDEGE WA TABATA?
WAJANE YATIMA WASINGECHOKA KUKUFUATA
WACHEZA KAMALI MAIMAMU NA MAPASTA
MGONJWA ANAOMBA APONE MAPEMA
WAKATI MUUZA JENEZA ALIKULILIA MAPEMA
MUUGUZI ANASEMA BABA HUYU MGONJWA USIMPONYE MAPEMA
NINASHIDA NA KIASI CHA HELA KWA AJILI YA MAMA
NAHISI UNGEHISI TUNAKUSAKAMA
KINA SISI TUNAOTAKA RIZIKI KWA KUCHANA
MWANAFUNZI ANALIA MIMBA ITOLEWE
WAKATI MGUMBA ANAKESHA MACHO NA MUMEWE
VIPI SASA MUNGU NDO UNGEKUWA WEWE?
KIFARANGA ANATEMBEA AKIKUOMBA WEWE
SIKIA MAOMBI JUU YA MWEMBE CHAKULA ANATAKA MWEWE
UNGEYASIKIA MAOMBI YA KICHAA?
AU UNGEKOMBA PESA ZOTE HALAFU UKAKESHA BAR?

RUDIA KIITIKIO

UBETI WA 3

UNGEFICHA SIRI ZAKO KAMA NGUO ZA NDANI?
AU TUNGEONA KILA KITU KA DAKTARI WA LEBA?
JE? UNGEYASIKIA MAOMBI YA KAHABA ANAYESALI KABLA YA TENDO UMUEPUSHE NA MIWAYA?
AU MWASHERATI ANAYEZUGA MWANAKWAYA?
UNGETUPA SHAVU KAMA MUNGU WA ISAYA?
MAANA BILA WEWE HAKUNA KALA WALA JEREMIAH
UNGESEMA HAYA,UNGEWAKUMBUKA WASUKUMAA NA WAHAYA?
VIPI LUGHA ZAO ZINGEPANDA HAWA WALA KAYA?
VIPOFU WANGEONA?AU UNGEDILI NA VIGOGO?
VIPI MADEM WA MJINI WENYE NYODO NA MIKOGO?
JE? UNGEICHOMA SODOMA NA GOMOLA?
AU NDO KWANZA UNGENOGEWA NA INSHU ZA MDUARA?
MAMBA ANA NJAA ANATAKA NYUMBU
NYUMBU ANAKUOMBA UMUONGOZE MTO USIO NA MAMBA
WAKULIMA WANALIA LETE MVUA JUU YA SHAMBA
DOBI NDO KATOKA KUANIKA NGUO JUU YA KAMBA
BILA MUNGU WE SIYO KITU ACHAA USHAMBA

RUDIA KIITIKIO

OUTRO
YAH THINK TWICE NATOKEA MWANZA.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment