OMMY DIMPOZ AFUNGUKA JUU YA KURUSHIWA CHUPA JIJINI DODOMA



Baada ya kutokea amesema sijasema, ni kweli ni uongo wiki iliyopita, kuhusu kutoa maneno ya dharau kwa Marehem Albert Mangweha a.k.a Ngwea, (ujinga wake umemfanya afe maskini), Ommy Dimpoz ametokea kupokea makopo na chupa akiwa stajini  (Kili tour) siku ya jumamosi ndani ya dodoma, Ommy alionekana steji akiwa anaimba na kukwepa makopo kwa wakati mmoja na baada ya kushindwa kuyavumilia aliamua kuachia stage na kushuka chini na mwisho kuondoka na kurudi hotelini alipofikia



leo hii kupitia xxl Ommy Dimpoz amezungumza juu ya situation hiyo

"ndio hivyo, nilikua nimepanda stajini, unajua kutokana na hili lililotokea, kwa hiyo tangia mwanzo hata mimi wenyewe nilijua labda kunaweza kukatokea fujo, lakini nilivyopanda watu walinipokea kuliko nilivyotarajai, kwasababu ndio tumetoka katika vugu vugu hili la, matatizo haya ambayo yamejitokeza sasa hivi.

kwahiyo ilivyofikia nimemaliza kuimba baadae, unajua hata kama kuna mtu alipanga kufanya fujo lakini ilikua sasa nguvu hata akipiga yeye akitaka kutumia nguvu ya watu wanaoshangilia ni wengi, ilipofika wakati naimba wa me and you, namalizia mwisho ndio kuna  baadhi ya mashabiki wakarusha makopostajini, lakini si unajua mimi mwenyewe nimepitia kumfuu kidogo kwahiyo nikayapangua, nilicheza nayo paaaaa paaaaaa.

imeenezwa chuki kwamba mimi nimemtukana marehem Albert kitu ambacho sio kweli, nimejaribu kukielezea kwenye media mbali mbali kuwa si kweli, wametumia kauli yangu niliyoongea kupitia Killi siku ya Tanzania Music Awards wakati kitu nilichokiongea nitofauti na kitu kilichokuja kupandikizwa, lakini mi najua safari ya mziki ni ndefu, na mwenyezi mungu atajaalia tu haya mambo yatakwisha kwasababu hata yeye mwenyewe anajua sina kosa, sija mkosea mtu wala sina tatizo na mtu, nafanya tu maisha yangu ya mziki, lakini inapofikia time unajua mtu mwingine anaweza akaja tu na sababu zake binafsi kwa nia ya kukuvuta shati, lakini kama mungu amendika njia yako nyeupe basi itakuwa nyeupe tu, na hakuna njia iliyonyooka siku zote lazima inakua na vikwazo kidogo, kwa hiyo naamini hii ni mitihani tu itaisha kwasababu sina tatizo na mtu.

nachoamini binaadam tunakufa pengine roho pengine zinabaki zina hang, hata marehem mwenyewe naimani anajua kwamba sikumtukana...................

hii ni challenge tu  naichukulia kwangu, pengine ni mitihani kwasabau sijawahi kuipata na  ku experience katika maisha yangu ya mziki hiki ni kitu kikubwa nimekutana nacho kwa sasa, lakini naimani itakwisha."
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment