VINEGA KUHUNGANA NA LADY JAY DEE


sugu,jide n profVita iliyoanzishwa na Mr II aka Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya kupitia tiketi ya chama pinzani cha CHADEMA juu ya unyonyaji na unyanyasaji wa wasanii wa mziki wa kizazi kipya huenda ikachukua sura mpya baada ya kundi la vinega kuungana na Lady Jay Dee katika vita yake dhidi ya Clouds FM.Vijana waliotoa maoni yao katika baadhi ya mitaa ya jiji la Dar Es Salaam ambako ndiko makao makuu ya Clouds FM na mahali ambako kuna wasanii wengi zaidi walisema huenda kundi la vinega likaungana na Lady Jay Dee na kufungua Radio yao ambayo itakua ni kama revenge kwa adui zao.
Hivi karibuni zimefanyika juhudi kubwa kunusuru wasanii kutumbukia katika umaskini wa kutupwa dhidi ya makampuni ya simu kunyonya kazi zao na upande wa pili baadhi ya radio ambazo zinaonesha upendeleo , unyanyasaji na unyonyaji wa wazi kwa kazi za wasanii.Clouds FM hivi karibuni imeshutumiwa na Lady Jay Dee kuendesha kampeni za kumuua kisanii ambapo pia imewalipa baadhi ya wasanii ambao walitakiwa kuhudhulia show ya Lady JayDee ili wasitokee katika shoo hiyo.Jamii haipendezwi na vita hii japo serikali imeonekana kufumba macho na kujifanya haioni kinachoendelea.Tuko pamoja katika kuona haki,usawa na amani vinatendeka.Mungu Ibariki Tanzania
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment