MTWARA HALI SIYO SHWARI
Habari zilizotufikia kutoka Mtwara zinaeleza kuwa kumeibuka vurugu ambazo zimepelekea mabomu ya machozi na risasi za moto kutumika baada ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa bungeni na kueleza kuwa mradi wa gesi Mtwara utatekelezwa bila kutaja faida za moja kwa moja watakazozipata wananchi hao. Inadaiwa kuwa kwa sasa kauli mbiu ya wananchi walio katika maeneo hayo ni "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni". Inaelezwa kuwa kituo cha mafuta cha Total kimechomwa moto wakati wa vurugu hizo. Katika kukabiliana na vurugu hizo, inadaiwa polisi kutoka Masasi na Lindi wapo eneo hilo kuongeza nguvu. Taarifa zaidi zitawajia hivi punde
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment