TUKO WANGAPIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

SOMA HII NA USHARE NA MWENZAKOO
NI KWELI NA YAMETOKEA JIHARADHII
NA HILI

Mimi ni Jane naishi mwenge Dar es
salaam naomba utalifuta jina la baba
yangu maana sitaki liwe kwenye blog
watu watanijua na kuniangamiza
maana nimeshawaangamiza wengi
sana kwa UKIMWI ila mengine yote
usifute hata moja ili dunia ijue tu
japokua mimi nitakufa kwa huu ukimwi
nilionao.
Nilizaliwa mkoa wa Dodoma na nilishi
vizuri tu tangu utotoni na hata
sikujihusisha na ngono hadi
nilipomaliza form 4 mwaka 2006 baada
ya kumaliza nilikuja hapa Dar kuishi
kwa mama mdogo aliyeolewa hapa
Mwenge.

Nilipata marafiki wengi tu na kuna
kijana mmoja alinitongoza kwa muda
mrefu sana na siunajua vijana wengi
hutumia muda mrefu kutongoza ili
msichana unadhani kwamba labda
huyo anakupenda kumbe anataka tu
ngono na wadada wengi sana hudhani
kufuatiliwa kwa muda mrefu na
mvulana basi huyo yuko serious
kumbe hakuna lolote.
Nilimkubalia tukawa wapenzi ila
nilikataa kuhusu kufanya mapenzi
maana anayekupenda kiukweli sio
uongo lazima asitake ngono kabla ya
ndoa.
Kwa miezi kama 5 hadi 6 aliniambia
kuhusu kufanya mapenzi nilikataa
alitumia mbinu nyingi sana kwa
kunibembeleza na hata kulia mbele
yangu ili tufanye tu mara moja ila
nilikataa, alisema atavumilia hadi siku
ya ndoa yetu ambapo tulipanga
kuoana mwaka sept 2009.
Siku moja aliniambia twende kwenye
kumbi za starehe na mimi kwa sababu
ya upagani na kumwamini pia kwa
sababu nampenda nilikubali tulienda
huko na kulikua na bendi fulani
maarufu ya mziki wa dansi ilikua
inatumbuiza.
Tulitafuta sehemu na kukaa na mpenzi
wangu akaagiza pombe alianza
kunywa huku akinionjesha, nilikataa
kwa sababu nilikua sijawahi kunywa
pombe katika maisha yangu yote, hata
sijui alinishawishi vipi nilijikuta
nakunywa kidogo kidogo na kwa kuwa
tulikaa pale kwa muda zaidi ya masaa 5
nadhani nikunywa kama bia 3 au 4
japokua nilikua nakunywa kidogo
kidogo tu tena kwa kunywesha na
mpenzi wangu maana nikama nikua
nanyweshwa kila baada kama ya dakika
25 ndipo nakunywa mara moja na
sikujuia kama nakunywa pombe ila
niliihisi tu naonja ili kumlizisha mpenzi
wangu.
Ilipofika saa 10 alfajiri nilihisi usingizi na
pia nilijiona wa tofauti najua nililewa
hata kama sikujua kama nimelewa
maana nakumbuka tulitoka pale huku
amenishika mkono huyo mpenzi
wangu. Tulikodo tax na kuondoka na
siku hiyo aliniambia twende kwake
alikokua amepanga chumba maana
tulikua na usingizi sana nilikubali huku
nikidhani hatuwezi kufanya mapenzi.
Tulifika salama na kuingia ndani ukweli
pombe ni kichocheo cha ngono na
ningekua mimi ndio Raisi wa Tanzania
ningefunga bar zote. Nilijikuta
natamani kufanya mapenzi na huyu
mpenzi wangu hata alikua hana nia
maana alijua atanichukiza sana na
uhusiano ungekufa siku hiyo lakini kwa
sababu ya pombe nilimwambia siku
hiyo tufanye kidogo maana mwili
wangu unataka.

Ni kweli siku hiyo kwa sababu ya
pombe nilifanya mapenzi na huyo
mpenzi wangu na baadae akanipeleka
nyumbani baada ya wiki mbili maana
tulikaa wiki mbili bila kuonana alikuja
na kunieleza habari ambayo sikuihitaji
katika maisha yangu maana nilikua
nasikia tu kwa watu wengine lakini sio
kwangu alisema ”JANE ISHI KWA
MATUMAINI KUANZIA SASA”
Nilidhani utani lakini aliniambia kuwa
yeye ana UKIMWI tangu miaka mitano
iliyopita na anapenda tu ngono maana
hawezi kuacha.

Nililia sana na baada ya wiki moja
baadae nikaenda kupima na kukutwa
nina ugojwa ambao niliusikia tu kwa
watu na chanzo cha yote ni pombe,
kupenda starehe,disko na upagani
unaotusumbua wanadamu wengi.

Nilikua na UKIMWI na kwa hasira
maana mpenzi wangu alihamia Arusha
huku akisema neno moja la mwisho
kwamba ”shetani amemtuma
kuwaambukiza wanadamu UKIMWI”
Sikujua, sikujua, sikujua,
sikujuaaaaaaaaa, basi tu ooh YESU
nihurumie mimi leo.Nilibebeshwa
mzigo ambao haukunistahili mimi.

Hata leo hua najiuliza kwamba
nilijitunza kwa miaka 23 yote lakini
pombe na huyu wakala wa shetani
wamenifanyia hivi. Baada ya kujua nina
UKIMWI na hali hiyo nikaikubali na
kulikua na kundi kubwa sana la
wanaume ambao walikua wamewahi
kunitongoja na niliwakataa sana kwa
sababu hii niliwakubali ili nami nife na
wengi.

Nilianza kumkubali kila mmoja na kuna
baba mmoja ambaye ana wake 3
niliwahi kumtukana sana kipindi cha
nyuma kila aliponitongoza lakini wakati
huu nilimkubali na hakuamini na
tukafanya ngono tena bila kinga na
akaniaachia pesa laki 6 kama zawadi ya
kumkubali kumbe naye hakujua kuwa
namwambukiza na hata leo hua
nawahurumia tu wale wake zake
ambao wana UKIMWI uliotoka kwangu.

Kiukweli tangu may 2009 hadi 2012
nimeshatembea na wanaume zaidi
1500 maana ilifika kipindi nala na
wanaume 3 kwa siku na lengo langu
niwakomeshe kama mimi
nilivyokomeshwa na nina uhakika
kutokana na mimi wameambukizwa
UKIMWI wanadamu zaidi ya 10,000 na
hili tangazo la ”TUKO WANGAPI” huwa
linaniliza kila siku maana hata mimi
najua kabisa nilianzisha mtandao kama
huo wa ngono kwa idadi kubwa sana
ya watu.

Nimeokoka miezi 7 iliyopita na siku
naombewa nilikutwa na mapepo
mengi sana na hata waombeaji
wakashangaa. Ningejua ningeokoka
tangu nikiwa na miaka 5 lakini ndio
hivyo sina jinsi wala uwezo wa
kubadirisha hali hiyo.

Na naomba kila atakayesoma ujumbe
huu ajue kuanzia leo kuwa pombe ni
dhambi pia kwenda disko ni
dhambi,kuuza pombe ni dhambi na
kila kichochoe chochote cha dhambi ni
dhambi. Hadi sasa mtu yeyote hawezi
kujua kama nina UKIMWI na sijui
MUNGU ana mpango gani na mimi
maana kwake yote yanawezekana.

Nauamini uponyaji wake na sijawahi
kutumia ARV hata siku moja na afya
yangu iko sawa tu na huwezi hata
wewe kujua kama uovu huu nimefanya
mimi.

Ndugu zangu kama una UKIMWI
nenda kanisani ukaombewe na kama
una akili mpe YESU maisha yako
maana pia baada ya kifo ni hukumu.
Yasalimishe maisha yako kwa YESU na
usiambukize wengine tena.

Mimi tangu niokoke sijawahi kufanya
mapenzi tena na sitafanya hivyo wala
sitaolewa na mtu yeyote maana
yatosha kwa uovu niliofanya na hadi
sasa wapo ninaowajua zaidi ya 15
wameshafariki na nilihudhulia misibani
huku nikijua kabisa chanzo ni mimi.

Mwisho nawashauli wababa kulidhika
na wake zao na wamama pia lidhikeni
na waume zenu, vijana ambao
hamjaoa wala kuolewa subiri hadi
utakapooa au kuolewa na kabla ya
kuolewa au kuoa kapimeni kwanza
kwani wenye UKIMWI ni wengi kuliko
unavyozani.

Fuata unachofundishwa kanisani na
pia soma BIBLIA na uwe mtakatifu.
MUNGU akubariki

Ni mimi Jane,
Mwenge, Dar es salaam
Tanzania
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment