Huku muziki, huku shule- Meninah



  Dar es Salaam. Mwimbaji wa ‘Dream Tonight’ Meninah Abdulkarim Atick amesema kuwa licha ya kuwa na mambo mengi, bado anaweza kuhimili mikiki ya shule pamoja na kutekeleza majukumu aliyopangiwa na wazazi wake.


Meninah ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari SJMC, alisema kwamba kwa sasa anajitahidi kuwa sawia kila pande, ili kupata baraka za wazazi wake.
“Mimi ni mwanamuziki, nina majukumu mengi. Karibu kila wiki nakuwa na safari za mikoani kufanya shoo, bado natakiwa kuhudhuria darasani,pia kusaidia wazazi wangu katika kazi mbalimbali nyumbani. Najipanga sana, nakabiliwa na mambo mengi,”alisema Meninah aliyeshiriki mashindano ya Epiq BSS mwaka jana na kuongeza:

“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha pamoja na kuwapa moyo wa subira wazazi wangu kwani wananiunga mkono katika kazi zangu za muziki.”
Msanii huyo anayeishi na wazazi wake Mikocheni jijini Dar es Salam, alisema kwamba licha ya yeye kuwa ni mwanamuziki anajitahidi kuwa katika maadili aliyofundishwa na wazazi wake, ikiwa ni pamoja na kujisitiri kimavazi.

“Navaa nguo za aina fulani nikiwa jukwaani na sehemu nyingine mara chache, lakini ukiniona siku za Ijumaa nakuwa tofauti kabisa. Ninachokifanya siyo kujificha kwa wazazi tu ila nazingatia maadili ya kujijengea heshima katika jamii,” anasema.

Meninah anayesomea Mawasiliano ya Umma katika SJMC, anasema kuwa wimbo wake ‘Dream Tonight’ amerekodi katika Studio za Saround Sound chini ya prodyuza Tudd Thomas.
Herieth Makwetta,
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment