
Wema Sepetu amepata ajali mbaya baada ya gari ambalo alikuwa
akiliendesha aina ya Audi Q7 kuacha njia na kugonga gari lingine kisha
kumgonga mtembea kwa miguu.
Tukio hilo ambalo lilivuta umati wa watu lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita maeneo ya Makumbusho, jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa Wema
alikuwa katika mwendo wa kasi na kushindwa kulimudu gari hilo
barabarani.
Ajali hiyo ilisababisha foleni na baadhi ya vijana wanaosadikiwa ni vibaka kuanza kumzingira.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyeomba hifadhi ya jina, inawezekana alikuwa na
mawazo mengi kichwani kwani licha ya kuwa kwenye mwendo wa kasi,
hakukuwa na sababu ya wazi iliyosababisha aache barabara.
“Yaani mi nahisi alikuwa na mawazo mengi au alikuwa ‘amepata’ kidogo,” alisema shuhuda huyo aliyedai aliona mchezo mzima.
Baada ya kugonga, ilidaiwa kuwa mwigizaji huyo alishuka kwenye gari na
kutaka kumpiga vibao mtembea kwa miguu huyo lakini ghafla watu
waliingilia kati na kumzuia huku wakimuonya kuwa akithubutu
wangemshushia kichapo.
“Huyu dada vipi? Ajali amesababisha yeye halafu anataka kumpiga mtembea
kwa miguu, angejaribu tu tungemvua nguo hapahapa,” alisema shuhuda mmoja
aliyekataa kuchorwa jina lake gazetini.
Hata hivyo, Wema alipomuona paparazi akiwa na vitendea kazi vyake
akimfuatilia kwenye gereji hiyo, aliondoa gari lake haraka ambapo umati
uliokuwa ukifuatilia kwa makini tukio hilo ulimzomea.
0 comments:
Post a Comment