Kweli
maisha hayatabiriki leo uko hai kesho haujui, Damino Damoche ambae ni
msanii na mwanafunzi wa Lagos State University (LASU) huko Nigeria,
hakujua kama maisha yake yatafikia mwisho kama yalivyofikia, jinsi
alivyopiga hiyo picha na rafiki yake ilikuwa ni muda mfupi kabla ya kifo
kibaya kilichomkuta msanii na mwanafunzi huyo.
Wala hakujua kama kifo chake kilikuwa karibu hivyo baada ya kutweet hiyo jana “Anticipate New Single Dropping Soon”. Msanii huyo ambae alikuwa anakuja kwa kasi na kufahamika katika kiwanda cha muziki Nigeria. Jana alipigwa risasi mbili kichwani na moja mkononi ilikuwa ni kwenye geti la chuoni (Lagos State University) alikuwa akitoka kufanya test ya mchepuo aliokuwa akichukuwa ya Management Science…Rest In Peace Damino Damoche.



0 comments:
Post a Comment